Total Pageviews

Tuesday, December 27, 2011

WADAU WA IDARA YA USHIRIKA BAGAMOYO

Jumamosi,
tarehe 24 Desemba 2011 wakati maandalizi ya X Mas yakiendelea kwa walio wengi, na ahueni ya maafa ya mafuriko ikianza kurejea taratibu, mimi na Mdau Herman Joseph tukawa njiani kuelekea Bagamoyo. Kwanza kuangalia athari za mafuriko kwa Mama Mkwe wangu Amina Kazinyingi aka Binti K pale Bagamoyo na pia kutoa salamu za pole kwa familia ya Rafiki na Ndugu wa siku nyingi Bw Hassan Salum Mirambo.
Kukaribia daraja la Kawe, tukapambana na mnyororo wa pande zote mbili, lakini nafuu iliyopo ni kuwa sasa panapitika angalau
Nyumbani kwa Binti K, athari za mafuriko zikiwa zimeicha nyumba hoi taabani japo maji yaliyoizingira sasa yakiwa yameondoka

Shukurani kwa mifereji ya dharura iliyotengenezwa kuondoa maji na kuyaongoza kwenye mfumo wake wa kawaida

Tukapata nafasi ya kufika kwa Mdau wa Idara ya Ushirika Bagamoyo, Bw Sango ili tuweze kufika pamoja kwa familia ya Bw Hassan Salum
Kwa joto la Bagamoyo ilikuwa kwanza kutafuta kivuli angalau ku cool down.

Baadae tulielekea kwa familia ya Hassan ambapo tulikaa nao kwa muda kiasi

(Kanuni za kimaadili zikanifanya nisichukue picha zozote pale chumba cha eda) Baadae tukapata nafasi ya kubadilishana mawili matatu pale Alpha Motel, palipoasisiwa na Marehemu George

Patrick Chomola na Herman Joseph
Juma Mwanambara in Blue kanzu

Shemeji Mubaraka, kulia






Hakika ni jambo la kushukuru Mungu kwamba sisi bado ametupa uhai.Kwa sababu katika dodosa dodosa zetu nilikuta kwamba tokea October 1982 nilivyoripoti kwa mara ya kwanza Idara ya Ushirika Bagamoyo, wenzetu wengi tuliowakuta wakatupokea au waliokuja baadae hawako nasi tena.

Mwenyezi Mungu uwapumzishe kwa amani wote waliotutangulia


  1. Mzee Mkodo

  2. Mujos

  3. Bruno

  4. James Wamalwa

  5. Mwakalinga

  6. Modibwa

  7. Godfrey Hassan

  8. Joseph Kabelwa

  9. Fatuma

  10. Hassani Salum

MUNGU UWAPUMZISHE PEMA PEPONI AMINA

Jioni tulipitia kwa rafiki BM Complex kubadilishana mawili matatu kabla ya majilio ya sikukuu

No comments:

Post a Comment