Total Pageviews

Wednesday, November 29, 2017

Tuesday, November 28, 2017

KISA CHA KALENDA

Hapo zamani,
Mwaka 1752, Waingereza walipokwenda kulala tarehe 2 Septemba lakini walipoamuka kesho yake ilikuwa tarehe 14 Septemba.
Kulikoni,
Siku 11 zilikuwa zimeondolewa kwenye Mwezi wa Tisa ili kuendana na Sheria mpya ya Kalenda.
"Calendar (New Style) Act of 1750"
Huu ni Mwezi Waingereza walihama kutoka matumizi ya Kalenda ya Julian kwenda Kalenda ya Gregorian.
Pia katika Kalenda ya Julian, mwaka mpya ukianza Tarehe 1 April. Sasa hata baada ya mabadiliko Waingereza wengi wakiendelea kusheherekea Mwaka Mpya April mosi. Kwa kuchukizwa na hilo Mfalme akawa ametoa amri kuwa wote wanaoendelea kusheherekea Mwaka Mpya April Mosi kuitwa Wajinga, Na kuanzia hapo April Mosi imejulikana kama Sikukuu ya Wajinga.

"Kutoka Mitandaoni"

Saturday, November 25, 2017

MAMA MKUBWA BIRTHDAY CELEBRATIONS

Photos from Mtwara Kwetu,
Hii na namna ilivyokuwa 16 Novemba 2017,
Wakati Bi Jennifer Simbua Bright akiadhimisha miaka kadhaa ya kuzaliwa kwake.

Friday, November 24, 2017

KINYEREZI KWETU

New Kinyerezi Bus Stand,
Panorama Photo shoot by Blogger

FOCONA RAFIKI WA MAZINGIRA MTWARA

Forum for Conservation of Nature, Mtwara HQ wanazidi kuchanja mbuga katika uhifadhi wa mazingira.
Pamoja na kuwa na Vitalu vya miti ambayo huisambaza baadae kwa jamii, Mitaani wameeneza ujumbe wa kuhimiza utunzaji wa Mazingira kama vile kutokutupa takataka ovyo na upandaji wa miti.

Thursday, November 16, 2017

Tuesday, November 14, 2017

UOGAJI KATIKA SAUNA

Wajua Sauna ni nini?
Sauna, kama Bafu la kuogea ni ustaarabu wa miaka mingi wa Watu wa Finland. Karibu kila nyumba nchini Finland in Sauna yake.
Hiki ni chumba maalumu ambacho hupashwa joto kwa Kuni, Mkaa, Umeme au Gesi kwa ajili ya kuweka Mvuke, Moshi au Joto kwenye Sauna.
Watu huingia humu kuoga mvuke, Mvuke huu husababisha mwogaji kutoa jasho. Na kwa kutoa jasho huamini mwili husafishika na kuimarika.
Sauna yaweza kutumiwa na mtu mmoja mmoja au watu wengi kwa pamoja, wa familia moja au ofisini
Kila nyumba, na kila Ofisi ina chumba cha Sauna
 Chumba cha Sauna, Turku University Science Park.

Friday, November 10, 2017

BAADA YA MVUA

Neema au Majanga?

MAMBO YA BARABARANI D'SALAAM

Ndio mambo ya Barabara zetu, Bongo Darisalama.
Ukitoka asubuhi nyumbani, Ukarejea Salama jioni,
Ni jambo la kumshukuru Mungu.
Matukio ya Majanga ya Barabarani Bongo ni kila pahala.

LIFE GOES ON

Mambo huja na kupita,
Baada ya Mvua za wiki zilizopita zilizosababisha mafuriko makubwa kwa wakazi wa Bonde la Mto Msimbazi, Dar sasa ni jua.
Hakuna Mafuriko,
Na Maisha yanaendelea.
Bonde la Msimbazi, Kawawa Road

ZA MWIZI 40

Kijana asiyejulikana, (katikati) akiwa amedhibitiwa kwa kufungwa Pingu, na kulindwa na watu wawili wasiojulikana akisindikizwa kuelekea pahala pasipojulikana.

Wednesday, November 8, 2017

ZEBRA CROSSING

Zebra Crossing,
Kivuko cha Barabarani kwa ajili ya waenda kwa Miguu.
Maarufu kwa nakshi yake ya Mistari Mieupe na Mieusi, mithili ya Punda Milia.
Kikilenga kuwa pahala salama pa kuvukia waenda kwa Mguu Duniani kote.
Lakini Je?
Madereva wetu wanaheshimu......
Vingunguti, Barabara ya Nyerere
Jumanne jioni.

KAMONGO

Mzigo umewasili,
All the way from Nakatuba,
Kamongo the Fish.

Tuesday, November 7, 2017

USWAZI KWETU

Uoto wa kijani unarejea baada ya siku chache za Mvua,
Bob, Wifi, Dizzo na Potta wanasherekea.

UTII BILA SHURTI!!

 Umekaa kwenye Foleni muda sasa,
Lakini anatokea Dereva wa Daladala asiye Muungwana,
Hawezi kutii sheria bila Shurti.
Yeye ana haraka zaidi............
Segerea Kinyerezi Road,
Jumanne asubuhi