Total Pageviews

Monday, February 29, 2016

PRESSURE YA NINI?

Ndio maana mara nyingi sipendi kuuangalia mechi zenye ushindani, Pressure ya nini Bana?
Hii ni mechi ya Liverpool na Manchester City Wembley jana usiku.
Hapa kuna Wanazi wa mpira, Man U, Liverpool, Arsenal na Chelsea.
Unaweza kuwatambua yupi ni yupi?

OUR PET

Wifi na Bob,
Kinyerezi kwetu, Jumapili

Saturday, February 27, 2016

Friday, February 26, 2016

ONCE UPON A TIME

What used to be a round about is now a crossing roads.
Uhuru rd/Msimbazi Street.

Thursday, February 25, 2016

AJALI NI AJALI

Guta limeacha njia na kupinduka jioni hii mitaa karibu na SDA Church, Ilala.
Hakuna aliyeumia.

PHOTO SHARING FROM HOME

Mzee wa mji visited home, and these are what he shared with us.

UTAMU WA SIASA

Mwanasiasa mkongwe nchini, Steven Wasira jana alimvamia na kutaka kumpiga mpigapicha wa gazeti la Mwananchi aliyekuwa akichukua picha zake wakati akitoka mahakamani.

Tukio hilo lilitokea jana wakati Wassira akitoka kwenye jengo la Mahakama ya Biashara ambako maombi yake ya kukata rufaa ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge, jimbo la Bunda yalitupwa na Mahakama Kuu.

Inadaiwa kuwa Wasira alimkimbiza Jamson akitaka kumnyang’anya kamera, lakini hakuweza na baadaye alitaka kumgonga kwa gari lake wakati akiondoka lakini ikashindikana.

Kwa mujibu wa Jamson (Mpiga picha) alisema Wasira, ambaye amefanya kazi na serikali za awamu zote tangu katikati ya miaka ya 70, alichukizwa na kitendo chake cha kumpiga picha.

“Wasira alinifuata na kuniuliza sababu za kumfuatilia kila mara. Aliniuliza picha nazopiga nazipeleka wapi,” alisema Jamson.

“Njoo, njoo hapa wewe kijana. Nakuambia futa hizo picha kwa usalama wako. Hivi mnatafuta nini maana mnanifuatilia tangu nikiwa kule Mahakama Kuu hadi huku Mahakama ya biashara,” alisema Wasira.

Wasira hakuishia hapo, katika kumfuatilia, gari la Wasira nusura limgonge mpigapicha huyo, lakini waandishi wenzake walimnusuru kwa kumsukumia pembezoni mwa barabara.
Awali, Jaji Sirilius Matupa alitupilia mbali maombi ya ruhusa ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa kufuta shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa Bunda baada ya kubaini waliowasilisha maombi hayo, Magambo Masato na wenzake wanne, hawakufuata sheria.
Uamuzi huo ulisomwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Eugenia Rujwahuka kwa niaba ya Jaji Matupa.
SOURCE:
Mitandaoni

Wednesday, February 24, 2016

ONLY IN BONGO !!!

Biashara katikati ya barabara, Lakini nani anajali?
Mtaa wa Mchikichini, Kariakoo leo asubuhi.

NAKATUBA SHOPPING, CONSTRUCTION PROGRESSING

Mwanasheria, Mzee wa Halamashauri, Mzee wa "Bhukoma" yuko Nakatuba.
Na leo ameshuhudia ujenzi unaoendelea wa Proposed shopping centre yetu.
Nakatuba leo asubuhi. 

Tuesday, February 23, 2016

Tuesday, February 16, 2016

KUWAFOTOA WAFOTOAJI

Kijiwe cha Ma"Photographer", picha Chap chap.
Msimbazi/Uhuru Street.

UMEWEKA ALAMA ?



Nimekumbuka leo kisa cha watu  wawili waliokwenda pahala kupitia mwitu mkubwa, Mmoja mwerevu mwingine mpumbavu. Mwerevu wakati wa kwenda alidodosha vipande vidogo vidogo vya mawe njiani, wakati wa kurudi vipande hivyo vilimsaidia kutambua njia ya kurudia. Mpumbavu alinyofoa vipande vidogo vidogo vya mkate na kuvitupa njiani alimopita, Kunguru walividonoa na kuvila, na wakati wa kurudi hakukuwa na alama yoyote, akapotea mwituni.
Dar Es Salaam nayo inabadilika haraka, kama huna alama zako huko mjini ipo siku utapotea.

Monday, February 15, 2016

CHANGING DAR

New "Ushirika Tower"
Lumumba, Mnazi mmoja.

BIASHARA UBUNIFU

Ama hakika biashara inataka ubunifu, Wauzaji mashine za kukatia mbogamboga.
Mtaa wa Swahili, leo mchana.

Monday, February 8, 2016

Sunday, February 7, 2016

MAJI YA SHINGO

Jumapili, masaa yanayoyoma......
Ukiangalia mambo ya Shuler Hayakawa sawa.
Unachohitaji ni elimu ya kujitegemea.
Kinyerezi kwetu, Leo Alasiri.