Total Pageviews

Wednesday, December 28, 2011

DOUBLE ANNIVERSARY 29 DEC

MIAKA 56 ILIYOPITA ALIZALIWA KULE NAKATUBA
Leo 29 DESEMBA ni Birthday ya Mdau
Mwl NYABHWANGU BELLY K MSALYA



Miaka 56 si haba, mdau akiwa PIDA akitafakari maisha haya


Nakatuba 2009

HAPPY BIRTHDAY DEAR BELLY Snr




Miaka mingi baadae mwanae mdau
GEORGE
anafunga ndoa na
LILIAN
tarehe
29 Desemba 2003



Na leo pia ni Kumbukumbu nzuri ya wadau hawa kwenye ndoa yao








TUNAWATAKIA MAISHA MEMA YENYE HERI MIAKA MINGI IJAYO








CK BIRTHDAY - KINYEREZI HIGHLIGHTS ZA MNUSO



























































































































































































































































TANZIA - KURURETERA NYAKUJERWA

Kururetera Nyakujerwa Maande

Taarifa zilizoifikia blog yetu, Ndugu yetu amefariki jana majira ya alasiri huko nyumbani Kisorya.

Mipango ya Mazishi inaendelea Kisorya.

Ndugu wa Dar Es Salaam tunataraji kukutana baadae jioni kuangalia namna ya kushiriki na kuwakilishwa.

HIVI NDIVYO NILIVYOIPITISHA SIKUKUU YA X MAS

Mapema asubuhi, siku ya sikukuu, Minoo, mimi na Manyama tukitafakari itakuwaje siku hii
Tukalazimika kuzuka dukani kwa Mangi, walau kupata mchele ili kubadilisha mlo wa sikukuu
mdau Issaya
Baadae Blogger akaingia kijiweni/masikani kwa stori za kupitisha muda
Mdau wa maskani

Huku tukivizia supu ya Kongoro ikiandaliwa

Stori kutoka kwa manazi wa mpira wa Uingereza zikiwa hazikosekani

Stori za hapa na pale na wajasiriamali



Na baadae mapema tukajisalimisha home kwa ajili ya kuwahi matukio muhimu kwenye Luninga kwa siku hiyo ya sikukuu, huku wadau wengine wakirejelea homeworks zao
Mungu ni Mwema, sikukuu imepita salama salimini.

Tunaisubiria Christmas ingine ijayo Mungu wetu akitujaalia

Tuesday, December 27, 2011

KARIBU MDAU JANETH

Msimu wa sikukuu hizi za X Mas na mwaka mpya safari hii zimetanguliwa na baraka kubwa
Mama Mdogo Salama amepata mtoto mzuri wa kike
JANETH MSENGI


Wadau wa Blog walipita kumuona Baby mapema kabla ya sikukuu
Blogger, Herman


HONGERA MAMA MDOGO SALAMA

KARIBU JANETH KWENYE BLOG YETU, NA ULIMWENGU WA DOT COM

WADAU WA IDARA YA USHIRIKA BAGAMOYO

Jumamosi,
tarehe 24 Desemba 2011 wakati maandalizi ya X Mas yakiendelea kwa walio wengi, na ahueni ya maafa ya mafuriko ikianza kurejea taratibu, mimi na Mdau Herman Joseph tukawa njiani kuelekea Bagamoyo. Kwanza kuangalia athari za mafuriko kwa Mama Mkwe wangu Amina Kazinyingi aka Binti K pale Bagamoyo na pia kutoa salamu za pole kwa familia ya Rafiki na Ndugu wa siku nyingi Bw Hassan Salum Mirambo.
Kukaribia daraja la Kawe, tukapambana na mnyororo wa pande zote mbili, lakini nafuu iliyopo ni kuwa sasa panapitika angalau
Nyumbani kwa Binti K, athari za mafuriko zikiwa zimeicha nyumba hoi taabani japo maji yaliyoizingira sasa yakiwa yameondoka

Shukurani kwa mifereji ya dharura iliyotengenezwa kuondoa maji na kuyaongoza kwenye mfumo wake wa kawaida

Tukapata nafasi ya kufika kwa Mdau wa Idara ya Ushirika Bagamoyo, Bw Sango ili tuweze kufika pamoja kwa familia ya Bw Hassan Salum
Kwa joto la Bagamoyo ilikuwa kwanza kutafuta kivuli angalau ku cool down.

Baadae tulielekea kwa familia ya Hassan ambapo tulikaa nao kwa muda kiasi

(Kanuni za kimaadili zikanifanya nisichukue picha zozote pale chumba cha eda) Baadae tukapata nafasi ya kubadilishana mawili matatu pale Alpha Motel, palipoasisiwa na Marehemu George

Patrick Chomola na Herman Joseph
Juma Mwanambara in Blue kanzu

Shemeji Mubaraka, kulia






Hakika ni jambo la kushukuru Mungu kwamba sisi bado ametupa uhai.Kwa sababu katika dodosa dodosa zetu nilikuta kwamba tokea October 1982 nilivyoripoti kwa mara ya kwanza Idara ya Ushirika Bagamoyo, wenzetu wengi tuliowakuta wakatupokea au waliokuja baadae hawako nasi tena.

Mwenyezi Mungu uwapumzishe kwa amani wote waliotutangulia


  1. Mzee Mkodo

  2. Mujos

  3. Bruno

  4. James Wamalwa

  5. Mwakalinga

  6. Modibwa

  7. Godfrey Hassan

  8. Joseph Kabelwa

  9. Fatuma

  10. Hassani Salum

MUNGU UWAPUMZISHE PEMA PEPONI AMINA

Jioni tulipitia kwa rafiki BM Complex kubadilishana mawili matatu kabla ya majilio ya sikukuu