Total Pageviews

Friday, December 2, 2011

MY 21 DAYS VACATION TO NAKATUBA - MJINI KIBARA

Welekeo ofisi ya mbunge wa jimbo la Mwibara. Ofisi hii japo sina hakika sana, itakuwemo kwenye jengo la CCM Kibara.
Mji wa Kibara una changamoto nyingi za kimaendeleo, ni mji wa muda mrefu ambao ukuaji wake umekuwa wa kusuasua. Miaka ya karibuni ulitangazwa kuwa mji mdogo. Na upimaji wa viwanja ukafanywa.

Kibara sasa inawasha stima, ingawa tatizo la maji limebakia palepele. Zamani zile tukifahamishwa ni uhaba wa mafuta ya mashine ya kusukuma maji. Leo je si kuna stima???

Jengo la CCM Kibara

Sina hakika kama kweli ni jengo la CCM au ni mali ya wananchi wote. Kwa maana zamani hizo likitumika kwa shughuli za wananchi wote. Nakumbuka 07.07.1967 tulikuwepo hapa sikukuu ya Sabasaba ukawepo ubwabwa kwa nyama ya Nyati. Kwa mahanjumati tuliyoyapata siku hiyo kesho yake nakumbuka tulirudi hapa tukidhania sikukuu inaendelea. Ni zamani sana sikumbuki tuliorudi nao siku hiyo.

Mambo ya mjini Kibara, Shalobalo Joshua mtaani
Mambo ya mjini,
Hapa ni kwa Mama Tereza
Joshua, Mama Tereza, Beria, Mama Nyasige na Nyang'oko
Chuma, Joshua, Mama Tereza, Beria na Zarau

Lake view from kwa manana

Kibara ina fukwe ndefu safi zinazofaa kwa uwekezaji wa shughuli za kitalii lakini fursa hii haijaonekana machoni pa wawekezaji.

Kibara kuna fursa ya ufugaji wa aina mbalimbali

Kwa "Nyamusarya" siyo "Msalya"

Kibara kama mji nao una vimbwanga vyake

Tuna changamoto ya stendi ya Magari ya abiria yafanyayo safari kupitia hapa

Stendi yetu Kibara

Walau sasa Kibara, kwa wale wa kilaji unaweza kupata Kili baridi, kuna sehemu chache za kupata vinywaji japokuwa hazijaanza kuchangamka kihivyo.
Tulipopata nafasi tulibadilishana mawazo kwenye vijiwe hivi.

Hapa ni Mr Jeremia aka Maradona na Shem Roba

Maradona na Ankal Suzy

Nani alisema Kibara hakuna Chips?

Ziko za kumwaga siku hizi.
Ankals Kevin, Joshua na Suzy wakithibitisha hilo siku walipotoka na Blogger

Nilikuwa nimekwisha jijengea kijiwe niwapo Kibara, na Kibara hakuna matata. Sikupata taabu ya kupata taswira hii kwani badala ya kuomba niwapige picha ilikuwa vice versa, wao waliomba niwapige picha kwa ajili ya kumbukumbu.

Miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika Kibara inakabiliwa na Changamoto nyingi.

Kiwanda kilichokuwepo hapa zamani hizo kimekufa, Hospitali iliyokuwa ikitukuka nje ya mipaka ya Kibara sasa ikichechemea.........

Sidhani kama tuna haja ya kuwarudisha wahindi.

1 comment: