Total Pageviews

Thursday, August 27, 2015

LIKE SON, LIKE DAD

Our selfie
Blogger with CK Junior (Crawford Kulwijira Kagere Msalya)
Kinyerezi kwetu, Jumapili.

TAKE CARE ROAD USERS

Barabara ni kwa watumiaji wa aina zote,
Na wote wanapaswa kuchukua tahadhari.
Ilala, Kanisa la Waadventista wasabato leo asubuhi.

NAMNA GANI YA KUINEZA INJILI

Kinyerezi leo asubuhi,
Muumini akiwajibika kueneza neno la Mungu.

Mathayo 28:19-20 "basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho mtakatifu na kuwafundisha kuyashika yote niliyo waamuru ninyi na tazama mimi nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari."

Wakolosai 1:26-29 "Siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake ambajinsio Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika mataifa nao ni kristo ndani yenu tumaini la utukufu amabaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu na kumfundisha kila mtu katika kila hekima yote tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika kristo Nami na jitaabisha kwa neno lilo hilo nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendaye kazi ndani yangu kwa nguvu."

Mathayo 24:14 "Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote hapo ndipo ule mwisho utakapokuja."

 1Wakorintho 2:1-5 "Basi ndugu zangu mimi nilipokuja kwenu sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno wala kwa hekima maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu kristo naye amesulibiwa nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na matetemeko mengi na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu bali kwa dalili za Roho na za nguvu iliimani yenu isiwekatika hekima ya wanadamu bali katika nguvu za Mungu."

 2Wakorintho 5:20 "Basi tuwajumbe kwa ajili ya Kristo kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu."

 Marko 16:15 na Yohana 13:35 "Akawaambia enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri injili kwa kila kiumbe... hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mikiwa na upendo ninyi kwa ninyi."

Isaya 60:1 "Ondoka ukaangaze kwakuwa nuru yako imekujia na utukufu wa Bwana umekuzunguka.

Isaya 61:1 " Roho ya Bwana Mungu I juu yangu kwa sababu Bwana amenitia mafuta ni wahubiri wanyenyekevu habari njema amenituma ili kuwanganga waliovunjika moyo kuwatangazia mateka uhuru wao na hao walio fungwa habari ya kufunguliwa kwao."

Wednesday, August 26, 2015

FROM THE ARCHIEVES OF NYACHIRIGA

Then Pte Nyachiriga Bright Msalya,  second left back row during Kagera War back in 1979.
Posing with Comrades at  Seventh Battallion,Tembo Brigade.
Right is the War Medal which he was awarded.

BONGO FILM PRODUCTION

Film production in Bongo has not been easy.
Bambo and his group shooting film in streets.
Msimbazi this afternoon

POLITIKI FAIL

Matokeo ya maamuzi mabovu ya wanasiasa.
Jengo hili la Soko lililokusudiwa kwa ajili ya wakazi wa kijiji cha Nakatuba na ambalo limegharimu mamilioni ya pesa za walipa kodi likiwa limetelekezwa bila kufanya kazi.
Aidha waliofanya maamuzi hawakujua Wananchi wa Nakatuba kipaumbele chao ni nini ? Au kama ni Soko basi lilipaswa kujengwa sehemu gani.
Bahati nzuri kwa wanasiasa hawa hakuna malalamiko kutoka kwa Wananchi, na wala hakuna wa kuwajibika kwa hasara hii.
Nakatuba kwetu hivi karibuni.

Monday, August 24, 2015

MICHEZO KWA AFYA

 utamu wa bao, kubadilisha mikao
 Hata Bao ni mchezo,
Na michezo ni mizuri kwa afya.
Mchezo wa bao ni bora sana kwa afya ya akili.
Kijiwe cha bao, Kibara Township
recently

EXPEDITION TO THE GREAT WALL OF NYACHIRIGA (3)

Obhutingo bhwa Nyachiriga
Blogger kazini
Pahala lilipokuweko Boma la Nyahiti, mstali mbele ya ukuta
Juu ya Ukuta
Mapambo Magesa, Paulo (Dreva wetu) na Nyachiriga
 Bw. John Mnyaga na Bw Nyachiriga Bright
 Bw. Mapambo Magesa na Bw Nyachiriga Bright
...............tuendelee..........


...........................................Kuufikia Ukuta wa Nyachiriga ni lazima kuvivuka vilima vitatu na mabonde yenye mtandao wa mawe mengi.
Baada ya kuvuka mfereji wa maji unaotenganisha Muchigondo na kisiwa cha Kubhwenyi, mita chache kufikia “Ukuta wa Nyachiriga” tunakutana na mwenyeji wetu mwingine, huyu ni Bw. John Mnyaga. Na yeye anaanza na kuhoji ujio wetu kwenye Ukuta huu.  Baada ya maelezo ya utambulisho ya hapa na pale huku tukimsisitizia kuwa hata kwenye msafara wetu, mmojawapo ni Nyachiriga Bw. John anaridhia kutusimulia kile anachokijua kuhusu “Ukuta wa Nyachiriga”.
Bw John Mnyaga anajitambulisha kama mkazi wa Muchigondo, Mkerewe wa ukoo wa Wasilanga. Utawala wa Chifu wa Ukerewe na Mwibara. Na wao ndio wenye haki ya umiliki wa ukuta huu wa kihistoria “Obhutingo bhwa Nyachiriga”.
Ukuta wa Nyachiriga unakisiwa ulijengwa kwenye miaka inayozunguka 1840, wakati wa utawala wa Nyahiti “Omkungu”, wa ukoo wa Wasilanga watawala wa himaya ya Ukerewe na Mwibara. “Omkungu” Nyahiti alijaaliwa kuoa wanawake Kumi na mmoja (11), kati ya hao Tisa (9) walimzalia watoto wapatao Tisini (90). Hata hivyo inaelezwa kwamba watoto Sitini (60) waliuawa wakati wa mapigano mbalimbali na maadui zao. Na dhana hii ndiyo chanzo cha kuwepo ujenzi wa Ukuta huu wa mawe kwa ajili ya kukinga Boma la “Omkungu” Nyahiti ambalo lilikuwa mita chache toka ukuta huu mkuu.
Kazi ya ujenzi wa Ukuta ilifanywa na Bw. Nyachiriga, kabila Mruri wa ukoo wa Abhatandu kutoka Efulifu, maeneo ya Bhururi/Bukwaya, Musoma. Ukuta huu upatao urefu wa mita 150, na kina cha mita mbili unaanzia mita 10 ndani ya maji upande wa Magharibi na kuishia mita kumi ndani ya maji upande wa Mashariki. Ni kazi ya kipaji na ustadi wa hali ya juu ambapo mawe yamepangwa kuwa Ukuta mrefu kuzuia maadui kwa nyakati hizo kulifikia na kushambulia Boma la “Omkungu” Nyahiti.
Bw John Mnyaga (1970) anasema yeye ni kizazi cha nne cha “Omkungu” Nyahiti, hata hivyo haelewi kwa nini Ukuta huu ukajulikana kama “Obhutingo bhwa Nyachiriga” – “Ukuta wa Nyachiriga” badala ya Nyahiti ambae kwa maelezo yaliyopo ndiye Mmiliki wa Ukuta. Hakuna maelezo ya kina pia kuhusiana na hatima ya “Omkungu” Nyahiti, hata hivyo inasemekana Himaya ya Wasilanga chini ya Chifu Rukumbuzya ina uhusiano wa karibu sana na utawala wa enzi za “Omkungu” Nyahiti.
 Kwa Nyachiriga pia hakuna maelezo mengi ya kina, hata hivyo inasemekana kuna kazi nyingine mbili tatu alizozifanya za ujenzi wa kuta kama huu huko sehemu za Bhururi na Ebhwenda, Majita japokuwa hazikuwa kubwa kama Ukuta huu uliopo kisiwani Kubhwenyi. Hatima ya Nyachiriga haijulikani pia, ingawa Bw. Mapambo Magesa mkaazi wa kijiji cha Nsunsi  tuliyekutana nae katika safari yetu hii anakiri kuwa yeye ni wa Mruri wa ukoo wa abhatandu, na ana Ndugu yake mmoja anaeitwa pia Nyachiriga aliyezaliwa mnamo mwaka 1945, ambae  ni mjukuu wa Nyachiriga Mjenzi wa Kuta.
Bila ya shaka makala hii itafungua njia kwa watafiti wengine wa kihistoria wa kizazi cha leo na kijacho kwa ajili ya kupata habari zaidi za Nyahiti na Nyachiriga kwa manufaa ya vizazi vijavyo vya eneo hilo la Muchigondo, Kubhwenyi na maeneo ya jirani kwa ujumla.

ZABURI 116:12 - NIMRUDISHIE BWANA NINI............

Jumamosi ya tarehe 08 August 2015,
Sehemu kubwa ya familia ya "Late" Crawford Kurwijira Msalya ilihudhuria ibada ya sabato katika kanisa Mama la Waadiventista Wasabato la Nakatuba.
Washiriki waliwasilisha salamu zao za kuguswa na Michango ya familia hii waliyoitoa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kanisa, Kundi la Nakatuba.
Ni matumaini yetu kuwa Mwenyezi Mungu atawezesha ukamilishwaji wa jengo hilo, kama ilivyokuwa ndoto za Baba yetu Mpendwa wakati anaumwa za kuona ujenzi huo unakamilika huku nae akishiriki kwa hali na mali.

ZABURI 116:12. “Nimrudishie Bwana nini Kwa ukarimu wake wote alionitendea?

Thursday, August 20, 2015

UK KUNA MAMBO !!

Please do not send letter to P.O. Box 496 Nansio.
Mambo ya Ukerewe hayo.

Wednesday, August 19, 2015

UTALII BILA KUTARAJIA


Utalii  wa bila kutarajia.
Gari tuliyokuwa tukisafiria kutoka Bunda kwenda Mwanza ilipata hitilafu tukiwa mbugani Serengeti.
Punde Nyani walijumuika nasi wakitafuta riziki kutoka kwetu.
Ni utalii wa ndani bila kuupangilia.
Hivyo kumalizia kwa kupata Lunch Villa Club ni utalii tosha wa siku hiyo.

EXPEDITION TO THE GREAT WALL OF NYACHIRIGA (2)

 Safari yetu inapaswa kufika pale..........
 Ni lazima kuvuka vilima na mambonde vyenye mtandao wa mawe mengi
Bw. Beka Lazaro Ng’oko (kushoto)


“OBHUTINGO BHWA NYACHIRIGA” Ikimaanisha “Ukuta wa Nyachiriga” ni mojawapo ya historia ya kipekee isiyojulikana sana, na inayokaribia kufutika.
Ijumaa ya terehe 07 August 2015, kwa ushawishi  wa Nyachiriga Bright K. Msalya ninapata bahati ya kuutembelea ukuta huu wa kihistoria kama mojawapo ya kujifunza na kupata maelezo kuhusiana na Ukuta  wa Nyachiriga.
Safari yetu kutoka nyumbani kwetu Nakatuba umbali wa kilometa 23 hivi, (30 km kutokea Kibara Centre) kuelekea kaskazini magharibi ikatupitisha katika vijiji vya Bhulendabhufwe/Mkoko, Mwigundu, Bhuguma na hatimae Muchigondo na kisiwani Kubhwenyi. Kubhwenyi ni kisiwa kidogo kinachotenganishwa na kijiji cha Muchigondo na mfereji wa maji (mto mdogo) unaounganisha maji ya ziwa upande wa Magharibi na upande wa Mashariki.
Mwenyeji wetu wa kwanza Muchigondo anakuwa Bw. Beka Lazaro Ng’oko tuliyesimama kumwomba maelekezo ya njia ya kuufikia Ukuta wa Nyachiriga. Beka mwenyeji wa Muchigondo na Bhuguma anatuthibitishia uwepo wa “Obhutingo bhwa Nyachiriga”, na anatusindikiza kwa umbali kidogo na kutuelekeza ramani namna ya kuufikia. Kuufikia Ukuta wa Nyachiriga ni lazima kuvivuka vilima vitatu na mabonde yenye mtandao wa mawe mengi.

Itaendelea.......................