Obhutingo bhwa Nyachiriga
Blogger kazini
Pahala lilipokuweko Boma la Nyahiti, mstali mbele ya ukuta
Juu ya Ukuta
Mapambo Magesa, Paulo (Dreva wetu) na Nyachiriga
Bw. John Mnyaga na Bw Nyachiriga Bright
Bw. Mapambo Magesa na Bw Nyachiriga Bright
...............tuendelee..........
...........................................Kuufikia Ukuta wa
Nyachiriga ni lazima kuvivuka vilima vitatu na mabonde yenye mtandao wa mawe
mengi.
Baada ya kuvuka mfereji
wa maji unaotenganisha Muchigondo na kisiwa cha Kubhwenyi, mita chache kufikia
“Ukuta wa Nyachiriga” tunakutana na mwenyeji wetu mwingine, huyu ni Bw. John
Mnyaga. Na yeye anaanza na kuhoji ujio wetu kwenye Ukuta huu. Baada ya maelezo ya utambulisho ya hapa na
pale huku tukimsisitizia kuwa hata kwenye msafara wetu, mmojawapo ni Nyachiriga
Bw. John anaridhia kutusimulia kile anachokijua kuhusu “Ukuta wa Nyachiriga”.
Bw John Mnyaga
anajitambulisha kama mkazi wa Muchigondo, Mkerewe wa ukoo wa Wasilanga. Utawala
wa Chifu wa Ukerewe na Mwibara. Na wao ndio wenye haki ya umiliki wa ukuta huu
wa kihistoria “Obhutingo bhwa Nyachiriga”.
Ukuta wa Nyachiriga
unakisiwa ulijengwa kwenye miaka inayozunguka 1840, wakati wa utawala wa
Nyahiti “Omkungu”, wa ukoo wa Wasilanga watawala wa himaya ya Ukerewe na
Mwibara. “Omkungu” Nyahiti alijaaliwa kuoa wanawake Kumi na mmoja (11), kati ya
hao Tisa (9) walimzalia watoto wapatao Tisini (90). Hata hivyo inaelezwa kwamba
watoto Sitini (60) waliuawa wakati wa mapigano mbalimbali na maadui zao. Na
dhana hii ndiyo chanzo cha kuwepo ujenzi wa Ukuta huu wa mawe kwa ajili ya
kukinga Boma la “Omkungu” Nyahiti ambalo lilikuwa mita chache toka ukuta huu
mkuu.
Kazi ya ujenzi wa Ukuta
ilifanywa na Bw. Nyachiriga, kabila Mruri wa ukoo wa Abhatandu kutoka Efulifu,
maeneo ya Bhururi/Bukwaya, Musoma. Ukuta huu upatao urefu wa mita 150, na kina
cha mita mbili unaanzia mita 10 ndani ya maji upande wa Magharibi na kuishia
mita kumi ndani ya maji upande wa Mashariki. Ni kazi ya kipaji na ustadi wa
hali ya juu ambapo mawe yamepangwa kuwa Ukuta mrefu kuzuia maadui kwa nyakati
hizo kulifikia na kushambulia Boma la “Omkungu” Nyahiti.
Bw John Mnyaga (1970)
anasema yeye ni kizazi cha nne cha “Omkungu” Nyahiti, hata hivyo haelewi kwa
nini Ukuta huu ukajulikana kama “Obhutingo bhwa Nyachiriga” – “Ukuta wa
Nyachiriga” badala ya Nyahiti ambae kwa maelezo yaliyopo ndiye Mmiliki wa
Ukuta. Hakuna maelezo ya kina pia kuhusiana na hatima ya “Omkungu” Nyahiti,
hata hivyo inasemekana Himaya ya Wasilanga chini ya Chifu Rukumbuzya ina
uhusiano wa karibu sana na utawala wa enzi za “Omkungu” Nyahiti.
Kwa Nyachiriga pia
hakuna maelezo mengi ya kina, hata hivyo inasemekana kuna kazi nyingine mbili
tatu alizozifanya za ujenzi wa kuta kama huu huko sehemu za Bhururi na
Ebhwenda, Majita japokuwa hazikuwa kubwa kama Ukuta huu uliopo kisiwani
Kubhwenyi. Hatima ya Nyachiriga haijulikani pia, ingawa Bw. Mapambo Magesa
mkaazi wa kijiji cha Nsunsi tuliyekutana
nae katika safari yetu hii anakiri kuwa yeye ni wa Mruri wa ukoo wa abhatandu,
na ana Ndugu yake mmoja anaeitwa pia Nyachiriga aliyezaliwa mnamo mwaka 1945,
ambae ni mjukuu wa Nyachiriga Mjenzi wa
Kuta.
Bila ya shaka makala
hii itafungua njia kwa watafiti wengine wa kihistoria wa kizazi cha leo na
kijacho kwa ajili ya kupata habari zaidi za Nyahiti na Nyachiriga kwa manufaa
ya vizazi vijavyo vya eneo hilo la Muchigondo, Kubhwenyi na maeneo ya jirani
kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment