Safari yetu inapaswa kufika pale..........
Ni lazima kuvuka vilima na mambonde vyenye mtandao wa mawe mengi
Bw. Beka Lazaro Ng’oko (kushoto)
“OBHUTINGO BHWA
NYACHIRIGA” Ikimaanisha “Ukuta wa Nyachiriga” ni mojawapo ya historia ya
kipekee isiyojulikana sana, na inayokaribia kufutika.
Ijumaa ya terehe 07
August 2015, kwa ushawishi wa Nyachiriga
Bright K. Msalya ninapata bahati ya kuutembelea ukuta huu wa kihistoria kama
mojawapo ya kujifunza na kupata maelezo kuhusiana na Ukuta wa Nyachiriga.
Safari yetu kutoka
nyumbani kwetu Nakatuba umbali wa kilometa 23 hivi, (30 km kutokea Kibara
Centre) kuelekea kaskazini magharibi ikatupitisha katika vijiji vya
Bhulendabhufwe/Mkoko, Mwigundu, Bhuguma na hatimae Muchigondo na kisiwani
Kubhwenyi. Kubhwenyi ni kisiwa kidogo kinachotenganishwa na kijiji cha
Muchigondo na mfereji wa maji (mto mdogo) unaounganisha maji ya ziwa upande wa
Magharibi na upande wa Mashariki.
Mwenyeji wetu wa kwanza
Muchigondo anakuwa Bw. Beka Lazaro Ng’oko tuliyesimama kumwomba maelekezo ya
njia ya kuufikia Ukuta wa Nyachiriga. Beka mwenyeji wa Muchigondo na Bhuguma
anatuthibitishia uwepo wa “Obhutingo bhwa Nyachiriga”, na anatusindikiza kwa
umbali kidogo na kutuelekeza ramani namna ya kuufikia. Kuufikia Ukuta wa
Nyachiriga ni lazima kuvivuka vilima vitatu na mabonde yenye mtandao wa mawe
mengi.
Itaendelea.......................
No comments:
Post a Comment