Mwanasiasa mkongwe nchini, Steven Wasira jana alimvamia na kutaka
kumpiga mpigapicha wa gazeti la Mwananchi aliyekuwa akichukua picha zake
wakati akitoka mahakamani.
Tukio hilo lilitokea jana wakati Wassira akitoka kwenye jengo la
Mahakama ya Biashara ambako maombi yake ya kukata rufaa ya kupinga
matokeo ya uchaguzi wa ubunge, jimbo la Bunda yalitupwa na Mahakama Kuu.
Inadaiwa kuwa Wasira alimkimbiza Jamson akitaka kumnyang’anya kamera,
lakini hakuweza na baadaye alitaka kumgonga kwa gari lake wakati
akiondoka lakini ikashindikana.
Kwa mujibu wa Jamson (Mpiga picha) alisema Wasira, ambaye amefanya kazi
na serikali za awamu zote tangu katikati ya miaka ya 70, alichukizwa na
kitendo chake cha kumpiga picha.
“Wasira alinifuata na kuniuliza sababu za kumfuatilia kila mara. Aliniuliza picha nazopiga nazipeleka wapi,” alisema Jamson.
“Njoo, njoo hapa wewe kijana. Nakuambia futa hizo picha kwa usalama
wako. Hivi mnatafuta nini maana mnanifuatilia tangu nikiwa kule Mahakama
Kuu hadi huku Mahakama ya biashara,” alisema Wasira.
Wasira hakuishia hapo, katika kumfuatilia, gari la Wasira nusura
limgonge mpigapicha huyo, lakini waandishi wenzake walimnusuru kwa
kumsukumia pembezoni mwa barabara.
Awali, Jaji Sirilius Matupa alitupilia mbali maombi ya ruhusa ya kukata
rufaa dhidi ya uamuzi wa kufuta shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa
Bunda baada ya kubaini waliowasilisha maombi hayo, Magambo Masato na
wenzake wanne, hawakufuata sheria.
Uamuzi huo ulisomwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Eugenia Rujwahuka kwa niaba ya Jaji Matupa.
SOURCE:
Mitandaoni
No comments:
Post a Comment