Total Pageviews

Saturday, November 5, 2011

MASKINI SHULE YANGU NAMALEBE

Maskini shule yangu Namalebe
Shule hii tunaambiwa ni shule kongwe Mwibara, ikianzishwa mnamo 1948
Kibao cha shule kilichochoka kama shule yenyewe, kikijinasibu kuwa shule imo kwenye wilaya ya kazi, Bunda - Maendeleo zaidi.
Vacation yangu ikanifikisha hapa baada ya miaka takribani 36 kupita toka nilivyoondoka shuleni hapa

Masikini Shule yangu Namalebe.
Enzi hizo Gofu hili lilikuwa ni nyumba ya Mwalimu

Walimu Martin na Sylivester walipata kuishi katika nyumba hii

Tukasimiliwa hakuna anaejali sasa, Mwalimu mmoja tu anaekaa na kufanya kazi zake hapa shuleni. Walimu wangine wapatao watano wanakuja kazini kwa kutokea wanapopajua wao.
Serikali imeitelekeza, na walimu wameikimbia
Nimesoma hapa 1967 - 1975
Wakati naanza shule, hii ilikuwa nyumba ya mwalimu mkuu, Mr Marko Riganya

Madarasa yetu, tuliyoshiriki kuyajenga miaka ya 1971 sasa yanaelekea kuwa magofu pia.
Hili lilikuwa darasa maarufu la LY

Tanki kwa ajili ya hifadhi ya maji kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi wawapo shuleni, tukilijenga kwa nguvu zetu pia

Darasa langu nililoanzia Class One, angalau sasa limekarabatiwa

Nikisoma hapa darasa la nne 1970, enzi za Mwl Pamba Haruna Seif Mkome, bingwa wa hesabu za kichwa. Na baadae Mwl Chibiriti

Class six, gofu sasa

LY 1973 - 1975

Hata sie choo chetu kilikuwa hapa hapa enzi hizo, overlooking Kilima cha Torokoko.

Wakati huo hakuna aliyethubutu kuingia kilimani hapo, lakini ukiniuliza kwa nini, sielewi hadi leo.

kuna madarasa mapya siku hizi

Nyumba ya Mwl Mkuu Eliab, mtaalamu wa Linguistic enzi zetu.

Mumewe Mwl Damali mtaalamu wa Hesabu kwa LY

Nyumba hii wakati naanza Class One akikaa Mwl Faustine Makaranga Ndimila.
Baba yao na Godfrey, Albert na Felista katika kukumbuka wachache.......

Ushiriki wa wanafunzi katika ujenzi wa shule yao, kumbukumbu hili tofali lilipigwa na Marehemu Baraka Magambo aka Charles Mtaju

Hili la "Chif" Rusasa, akikaa kwa mzee Matekere

Upandaji miti bado unaendelezwa , inapendeza sana

Na angalau baadhi ya madarasa sasa yana madawati

Kuna nyongeza ya madarasa mapya, yenye mvuto mpya
labda ndiyo maana yale ya kizamani hawana haja nayo tena hata kwa kuyakarabati

Mvuto mpya

Hapa usiombe kufika enzi hizo, ndiyo iliyokuwa staff room ya Walimu.
Dirisha kushoto ikiwa ni Maktaba ya Shule ambayo nami nikipata bahati ya kutumika hapo kipindi fulani

Staff Room

Nikaikumbuka plot yangu ya usafi
Enzi hizo za viranja wetu, Nyande Missana Mkhoi, Daudi Mkani na wengineo...

Mlango huu ndipo nilipomalizia masomo yangu ya shule ya msingi 1975

Shukrani sana kwa Mwl Jackson kwa niaba ya walimu wote waliopo na waliowahi kupita Namalebe.Ziara yangu hapa imenikumbusha mbali.

1 comment:

  1. Namalebe na Nakatuba kwa ujumla zimekwisha sana. Pole S/M Namalebe

    ReplyDelete