Bw. Phillipo Malekela
Mwaka 1946, wakati Mzee Magoti Kubhoja anafikwa na umauti kwa ajali ya
kushikwa na Mamba, alimwacha Mjane Bi. Nyamambala Mweya akiwa mjamzito. Lakini
pia akiacha watoto sita. Kaitira, Nyamitaga, Maingu, Nyabhutwema, Mnubhi na
Tereza. Muyabhi ambaye hakupata bahati ya kumuona Baba yake Mzazi uso kwa
macho.
Changamoto kubwa ya kimaisha kwa familia hii ilikuwa inaanza mkondo
mpya. Kaitira kijana mkubwa wa familia hakuwa ameoa, hivyo jukumu la kuwa
kiongozi mkuu wa familia lilikuwa kubwa mno kwake. Bahati mbaya pia Magoti
hakuwa na ndugu wa karibu upande wa Baba. Kutokana na utata wa kifo chenyewe,
Mitizamo tofauti ya chuki kati ya familia ya Magoti na ile ya kina Temburu
ilikuwa sasa ni dhahiri. Familia ya Magoti ilipaswa kuondoka mahala mara moja
baada ya mazishi.
Mwisho wa historia ya Familia ya Magoti kijijini Namibhu.
Kwa upande wa Mama, Magoti
akizaliwa na Nyang’oko Malandala. Nyag’oko akizaliwa pamoja na mdogo
wake Nyamtondo Malandala. Nyamtondo ndiye Mama Mzazi wa Malekela Nyachemo.
Naam, familia ya Magoti ilikuwa inaanza historia mpya ya Maisha Kijiji
cha Nakatuba nyumbani kwa Malekela Nyachemo. Hapa kwa Mzee Malekela wanakutana
na watoto waliokuwa wamekwisha zaliwa ambao ni Rhudia, Stephano na Nyabhwire.
Baadae kwa Mama Nyamabhusi walikuja kuzaliwa Damali na Tabitha.
Tabitha Malekela, Kasahunga
Baadae pia Mzee Malekela alilazimika kurithi familia ya Mjomba wake
Mukama aliyefariki. Bi Nyalulinga alirithiwa na mpwa wa mmewe. Alikuja na
watoto Matofari, Muinja na Nyanjura. Na baadae kwa Bi Nyalulinga walizaliwa Daudi na Philipo.
Tereza alikaa muda mchache Nakatuba kabla ya yeye kwenda kulelewa
Mwitende .
Mnamo mwaka 1949, Ilianzishwa shule ya Msingi ya Nakatuba. Wananchi
walihamasishwa kupeleka watoto wao kujipatia elimu. Mzee Malekela aliridhia
Mnubhi na Nyabhwire kuandikishwa shule. Wengine walionekana wadogo na wengine walioonekana
wakubwa aliona ni akiba ya nguvu kazi. Hii ndiyo sababu mji mmoja wengine
walienda shule na wengine hawakwenda.
Mnubhi baada ya kumaliza darasa la Nne Namalebe , alipata kusoma
Mabhuimerafuru, Ukerewe na baadae Uganda.
Nyabhwire alifanya vizuri mitihani yake ya darasa la Nne, akachaguliwa
kwenda darasa la tano na sita shule ya Bwiru jijini Mwanza.
Maingu baadae alielekea Iramba
kwa Mzee Rwanda, huko alifanikiwa kuanza shule iliyompeleka hadi Bukhima na
kufanikiwa kumaliza darasa la nne.
Nyamitaga na Nyabhutwema waliolewa wakitokea nyumbani kwa Mzee
Malekela. Maingu akimuoa mkewe Nyamkaruka akiwa kwa mjomba wake Mzee Rwanda.
…….mkondo mpya wa familia ya Magoti, kila mmoja na maajaliwa yake…………………………………
These are wonderful stories that should be compiled and keep in durable record facilities to be read by many generations in future.
ReplyDelete