Kaitila Magoti Kubhoja, The first born- Mabhuimerafuru
Mrs Nezia Maingu Magoti - Karukekere
Tereza Magoti (Mrs Wilson Kuruchumila) - Kibara
Nyamaira kubhoja na Magoti Jnr (Blogger) - Igundu
Nyamitaga Neema Magoti (Mrs Chisute Mteki) - Bhulinga
Ernest Munubhi Magoti - Mabhuimerafuru
Nimekuwa nikitatizwa,
Simulizi zimekuwa zikieleza Magoti Kubhoja alikuwa na maskani yake
Kibara, Namibu hadi alipokutwa na mauti.
Kaitila Magoti, mwanae wa kwanza maskani yake yako Mabhui Merafuru hadi
leo, na Maingu Magoti maskani yake hadi anapatwa na mauti yalikuwa Karukekere,
Chingurubhira.
Karibuni nilipata likizo ambayo ilinifikisha hadi Igundu, Majita Mabhui
Merafuru na Karukekere, na nilipata nafasi
ya kudodosa kutoka kwa watu wa familia yake kulikoni wanae kuacha pahala
pa asili!
Tafadhali fuatana nami katika simulizi hii ya Bw Magoti Kubhoja.
Hakuna tarehe kamili ya kuzaliwa kwa Magoti, lakini inakisiwa kuwa
huenda alizaliwa kwenye miaka ya mwanzo ya karne ya 19. Alizaliwa katika kijiji
cha Ekome na kukulia hapo miaka ya awali. Hakuna hakika ya asili yao, japo
kulikuwa na fununu kuwa chimbuko lao hasa walitokea Buhaya. Lakini amekua
akijulikana kama Mjita Mkome, ukoo wa Abhakura
– Wa kutoka mbali.
Wakati wa ujana wake, Magoti alipendelea kwenda kukaa Iramba, Sikiro
kwa mjomba wake Bw. Mukama Marandara, kaka yake na Nyang’oko. Inasimuliwa
kwamba siku moja Shangazi zake akiwepo mmoja aliyeitwa Nyamtondo walikwenda
kumtembelea Kubhoja huko Ekome.
Hawakupendezwa kumuona Kaka yao akijiandalia kukoka moto wa jioni “Echoto” kwa
kuwa Magoti hakuwepo. Waliahidi kumshughulikia. Huko Sikiro Magoti alikosa
nguvu za kiume na akalazimika kurejea Ekome kwa matibabu.
Miaka mingi baadae baada ya kifo cha Kubhoja alirejea Iramba,Sikiro, lakini safari hii hakukaa sana
kwa sababu alishawishiwa na Binamu yake Bw. Temburu mtoto wa shangazi yake
Nyakalolo kwenda kuishi Namibu jambo aliloliridhia wakaongozana kwenda huko ambako
Temburu alimpatia mashamba. Akiwa Namibu Bw Magoti alimwoa Nyamkubhi Bhulilo
mkazi wa Majita Bhutata. Ni wakati huu kulipoanza kujitokeza tofauti kati yake
na Binamu yake hivyo akawa amedhamiria kuanza mji wake.
Kwa upande wake Bw Temburu pamoja na kuoa mapema hakuwa amejaaliwa
kupata watoto. Na katika kuhangaikia kupata watoto alifika hadi kwa waganga wa
Kikara waliokubali kumsaidia ila kwa kumtoa kafara nduguye wa karibu, Temburu
aliridhia kafara yake kuwa Bw. Magoti.
Magoti baada ya kuanza kuwepo
kwa tofauti na binamu yake Bw. Temburu alikuwa amedhamiria kuanzisha mji
wake. Siku moja katika maandalizi ya ujenzi wa mji wake alikuwa amepanga na
shemeji yake mme wa Nyamaira “Nyakubhoja” kuwa
angemletea baadhi ya vifaa vya kusaidia ujenzi kesho yake. Aliamua yeye
na mwanae Maingu kwenda ziwani jioni hiyo kuwatafutia mboga ya kesho yake,
Hakurejea tena.
Wakiwa uvuvini, Magoti aliopolewa na Mamba kutoka mtumbwini akimwacha
Maingu pekee. Habari zilisambaa na jitihada zikafanyika usiku kucha kumtafuta
huyo Mamba mla watu. Hakupatikana.
Lakini kesho yake maiti ya Magoti ilipatikana ufukweni mwa ziwa ikiwa
na majeraha ya damu. Ikiwa imerudishwa na Mamba mla watu, na ndio ulikuwa
mwisho wa Magoti Kubhoja. Mnamo mwaka wa 1946.
Miaka ya baadae Temburu alifanikiwa kupata watoto, Mmoja wao maarufu
kama Mwinyi Temburu anaendelea kuishi
maeneo yaleyale yaliyoachwa na Temburu na Magoti pale Kibara Namibu hadi leo.
………………………………………………………fuatana
nami wakati mwingine……….
No comments:
Post a Comment