Tuna na paswa kufanya nini wakati mauti yako machoni mwetu? Ikiwa Mungu
yu pamoja nasi tusiwe na hofu imeandikwa Zaburi 23:4 "Naam nijapopita
kati ya ponde lauvuli wa mauti sitaogopa mabaya kwa maana wewe upo
pamoja nami gongo lako na fimbo yako vyanifariji."
Kifo kinafanana vipi? Nikama usingizi. imeandikwa 1Wathesalonike 4:13
"Lakini ndugu hatutaki msijue habari za waliolala mauti msije
mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini." pia Yohana 11:11-14
"Iliyasema hayo kisha baada ya hayo akawaambia, rafiki yetu Lazaro,
amelala lakini nitakwenda nipate kumwamsha. Basi wale wanafunzi
wakamwambia Bwana ikiwa amelala tapona lakini Yesu alikuwa amenena
habari ya mauti yake nao walidhani yakuwa ananena habari ya kulala
usingizi. Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi Lazaro amekufa."
Danieli amesema nini kuhusu kifo? Imeandikwa Danieli 12:2 "Tena wengi
wahao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka wengine wapate uzima wa
milele wengine aibu na kudharauliwa milele."
Je? walio kufa wanajua lolote? Imeandikwa Mhubiri 9:5-6, 10Kwa sababu
walio hai wanjua ya kuwa watakufa lakini wafu hawajui neno lolote wala
hawana ijara tena maana kumbukumbu lao limesahauliwa mapenzi yao
namachukio yao na husuda yao imepotea yote pamoja wala hawana sehemu
tena katika jambo lolote lililofanyika chini ya jua, lolote mkono wako
utakapolipata kulifanya ulifanye kwa nguvu zako kwa kuwa hakuna kazi
wala shauri wala maarifa wala hekima huko kuzimu uwendako wewe."
Kifo sio mwisho! Imeandikwa Isaya 26:19 "Wafu wako wataishi maiti zako
zitafufuka amkeni kaimbe ninyi mnao kaa mavumbini kwa maana umande wako
nikama umande wa mimea nayo ardhi itawatoa waliokufa."
Yesu ametuhaidi nini kuhusu kifo? imeandikwa Hosea 13:14 "Nitawakomboa
na nguvu za kaburi nitawaokoa na mauti ewe mauti yawapi mapigo yako? Ewe
kaburi ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafishwa na macho yangu."
Ufufuwaji uko katika nguvu za Mungu imeandikwa 1Wakorintho 15:21-22
"Maana ya kuwa mauti ili letwa na mtu kadhalika na kiyama ya wafu
italetwa na mtu kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa kadhalika na
katika Kristo wate wanahuishwa."
Mungu alimpa mwanawe kwa sababu gani? imeandikwa Yohana 3:16 " Kwa maana
jinsi hii Mungu aliupenada ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee ila
kila amwaminiye asipotee bali awena uzima wamilele."
Watu wema na wabaya watafufuliwa siku ya kiama imeandikwa Yohana 5:28-29
"Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote walio
makaburini wataisikia sauti yake nao watatoka wao waliofanya mema kwa
ufufuo wa uzima na wale walio tenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu".
Waaminifu watafufuliwa yesu akirudi mara ya pili imeandikwa
1Wathesalonike 4:16-18 "Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka
mbiguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu na parapanda ya
mungu nao walio kufa katika kristo watafufuliwa kwanza kisha sisi tulio
hai tuliosalia tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu ili tumlaki Bwana
hewani na hivyo tutakuwa na Bwana milele. Basi farijianeni kwa maneno
hayo."
Tutafanana vipi baada ya ufufuo? Imeandikwa Wafilipi 3:20-21 "Kwa maana
sisi wenyeji wetu uko mbinguni kutoka huko tunamtazamia mwokozi Bwana
wetu yesu kristo atakaye ubadili mwili wetu wa unyonge upate kufanana na
mwili wake wa utukufu kwa uweza ule ambao kwa huo uweza hata kuvitiisha
vitu vyote viwe chini yake."
Watakatifu wataishi mda gani? imeandikwa Luka 20:36 "Wala hawawezi kufa
tena, kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa
vile walivyo wana wa ufufuo."
Wenye dhambi wta ngoja kwa mda gani kabla ya kiama? imeandikwa Ufunuo
20:4-5, 9 "Kisha nikaona vitu vya enzi wakaketi juu yake nao wakapewa
hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya uchuhuda wa
Yesu... Hao walio wafu salia hawakuwa hai hataitimie ile miaka elfu,...
9 Moto ukachika toka juu mbiguni ukawateketeza."
Wenye dhambi ni nani? imeandikwa Ufunuo 21:8 "Bali waoga, wasioamini,
wachukizao, wauwaji, wazinzi, wachawi, waabuduo sanamu, na waongo sehemu
yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti, hiyo ndiyo mauti ya
pili."
No comments:
Post a Comment