HISTORIA FUPI YA
CRAWFORD KURWIJIRA MSALYA. “CK”
04 Januari 1931 – 26 September 2014
Kurwijira
Crawford Msalya alizaliwa tarehe 04 Januari 1931, Kijijini Nyambubhi,
Kisorya Bunda wakati huo ikiitwa wilaya
ya South Mara. Baba yake akiitwa Msalya Maseme “Sekaseka” na Mama Bhituro
Msema.
Mwaka 1937
Mzee Msalya alihama na familia yake kutoka Nyambubhi kwenda Nakatuba, Mwibhara.
Tokea mwaka
huo hapa ndio pamekuwa makazi yake Bw Kurwijira Crawford Msalya.
FAMILIA.
Marehemu
Kurwijira alimwoa Bi. Nyabhutwema Penina Magoti tarehe 17 Novemba 1951, ambae
walijaaliwa kupata watoto kumi na mbili, watoto walio hai leo ni watoto kumi.
Belly
Bright
Billy
Beria
Baruku
Bithia
Bora
Bahati
Bilshani na
Baasha
Marehemu
Kurwijira amebahatika kupata wajukuu 34, lakini hadi anafariki ameacha wajukuu
30 walio hai.
Marehemu pia
amebahatika kupata vitukuu wanane.
Peter CK
Penina
Belly
Pricilla
Billy
Miriam
Poulsen
BenGeorge.
Marehemu
amefariki akiwaacha wadogo zake watatu kwa kuzaliwa.
Mwayai
Chausiku
Tabhu
IMANI
Mzee
Kurwijira alibatizwa mwaka1989 na Mchungaji Makoko katika kanisa la
Waadivenista Wasabato Nakatuba, na amekuwa mshiriki hapo hadi mauti inamkuta.
ELIMU NA UTUMISHI
Marehemu
alipata elimu ya msingi kati ya mwaka 1944 hadi 1950 katika shule mbalimbali za
Kitengule SDA (Paul School), Bunere SDA, Elusori, Bwasi na Nyambitilwa
(Ushashi).
Utumishi
wake ulikuwa katika Nyanja tofauti tofauti.
·
1952 – 55, Karani South Mara Native Authority
·
1955 - 57,
Karani wa Mahakama, Ushashi – Utemi wa Chifu Masanja.
·
1957 – 61, Karani Namalebe Growers Cooperative
Society
·
1975, Afisa Ulinzi MICO
·
1975 – 84, Bwana Shamba Mamlaka ya Pamba
Tanzania, Mara
SIASA NA JAMII
Marehemu
Mzee CK ametumikia pia nyadhifa mbalimbali za kisiasa na kijamii.
·
1955, alijiunga na chama cha TANU
·
1958, Kuingia TANU Youth League
·
1977, Kujiunga na CCM
·
1965 – 67, Diwani South Mara District Council
·
1968 – 75, Mwenyekiti wa Kijiji Nakatuba/Kata
·
2000 – 04, Mwenyekiti TASAF Nakatuba
·
1997 – 2005, Mwenyekiti CCM Kata ya Kibara
Pia Mzee CK
kwa nyakati mbalimbali aliwahi kutumikia nyadhifa nyingine kati ya miaka ya
1958 na 1970, ambazo ni pamoja na:
o
Mjumbe Kamati ya Tawi la TANU Kibara
o
Mjumbe, Kamati ya fedha na DDC ya Baraza la
madiwani
o
Katibu na mjumbe, Umoja wa Vijana Tawi la Kibara
o
Mjumbe wa nyumba kumi
o
Mjumbe wa Kanda, Chama cha Ushirika Nyanza
o
Mjumbe wa Tanu Wilaya na Mkoa
o
Mwenyekiti wa TANU Kata ya Kibara
o
Mzee Mshauri, Mahakama ya Mwanzo Nansimo
o
Karani Baraza la Usuluhishi, Kata ya Kibara
o
Mwenyekiti Shule ya Msingi Kitengule
o
Mwenyekiti shule ya Msingi Namalebe
o
Mwenyekiti Chama cha Ushirika cha Msingi,
Nakatuba
o
Mjumbe, Chama kikuu cha Ushirika Mara, Mara Coop
o
Mwenyekiti Baraza la Kimila Nakatuba
o
Mjumbe wa CCM, Mkutano mkuu wa Wilaya na Mkoa
Maradhi ya
Mzee CK yalianza kujitokeza Desemba 2013, wakati huo akiwa ametembelewa na
wanae na wajukuu nyumbani Nakatuba aliwasimulia tatizo alilo nalo la maumivu wakati
wa kumeza chakula.
Kati ya
mwezi Desemba 2013 na Januari 2014 alipata matibabu ya awali katika hospitali
ya Mkombozi iliyopo mjini Bunda.
Mnamo April
2014, Mzee CK alianza safari ya kuelekea Dar Es Salaam kwa ajili ya matibabu
akipitia Bunda, Mwanza, Dodoma na
Morogoro. Akiwa Morogoro alipata vipimo na uchunguzi katika Hospitali ya mkoa
ya Morogoro. Hakuna tatizo lolote lililogunduliwa.
Mzee CK
aliendelea na na vipimo vya uchunguzi katika Hospitali za Madona na baadae
Tabata General Hospital ambao waligundua kuwepo kwa kwa tatizo la uvimbe kooni.
Tatizo ambalo lilithibitishwa tena katika Hospitali za Hindu Mandal na Besta
Diagnosis Kinondoni na ikashauriwa na Madaktari afanyiwe upasuaji.
Alilazwa
Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe
tarehe 27 April 2014, ulioongozwa na Dr Mavura akisaidiana na Dr Katembo.
Ilipendekezwa baada ya muda afanyiwe upasuaji wa pili kwa ajili ya kurejesha
mfumo wa kawaida wa chakula.
Tarehe 27
May 2014 alilazwa tena Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na akafanyiwa upasuaji
wa pili tarehe 30 May 2014, Upasuaji ambao haukufanikiwa na ikapendekezwa
aendelee kubakia kwenye uangalizi wa madaktari wa mara kwa mara kwa ajili ya
kufanyiwa upasuaji wa tatu. Bahati mbaya wakati akiendelea kusubiria upasuaji
huo afya yake ilikuwa ikiendelea kuzorota siku hadi siku. Pamoja na jitihada za
uangalizi na uimarishaji wa hali yake, haikusaidia. Kuanzia tarehe 20 Septemba
2014 hali ilianza kudhoofu kwa kasi hadi mauti ilipomkuta tarehe 26 Septemba
2014, Saa moja na dakika tano jioni nyumbani kwa Mjukuu wake Bw Eddyson Msalya.
Mzee CK alikata roho mbele ya familia yake, Mkewe Bi Penina, Mdogo wake Bw Mwayai
na wanae Billy, Bilshani, Sarah na Beria.
Bwana
alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
AMINA
No comments:
Post a Comment