Total Pageviews

Wednesday, November 20, 2013

MTENDAJI ANUSURIKA KIFO AKIDAIWA KUIBA MAHINDI BUNDA.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Joshua Mirumbe
Na Masau Bwire, Bunda.
OFISA Mtendaji wa Kata ya Iramba, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, Simon Katikizu,
amenusurika kifo baada ya wananchi wenye hasira kumshambulia kwa mawe
wakimtuhumu kuiba mahindi ya msaada.
ni Makao Makuu ya kata hiyo ambapo wananchi walikusanyika ili kugawiwa mahindi
ya msaada.
Tukio hilo lilitokea juzi saa 4 asubuhi, Kijiji cha Isanju ambacho 
ni Makao Makuu ya kata hiyo ambapo wananchi walikusanyika ili kugawiwa mahindi
ya msaada.
Wakati kazi ya kugawa mahindi hayo ikiendelea, wananchi hao walibaini upotevu wa
magunia zaidi ya 40 na baada ya kufanya uchunguzi, wakagundua wizi huo
ulifanywa na Bw. Katikizu 
hivyo walianza kumshambulia kwa mawe na marungu.
“Tumemkamata na mahindi ya msaada akiwa ameyaficha nyumbani kwake, katika Ofisi
ya Elimu, kilimo na mengine aliyaweka katika nyumba za rafiki zake, wakati
akijaribu kukimbia lilipigwa yowe,” alisema Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
CCM, katika kata 
hiyo, Mohamed Gamba.
Alisema Serikali ilipeleka msaada wa magunia 318 ya mahindi
kwa ajili ya vijiji vitano vya kata hiyo ambapo kila kijiji kilipaswa kupata
magunia 63 kutokana na njaa inayowakabili wananchi.
Vijiji vilivyokumbwa na tatizo la njaa ni Isanju, Mugara, Sikiro, Nyarugoma na
Mwiruruma, lakini. Katikizu aliiba kiasi kikubwa cha mahindi ambapo kijiji cha
Nyarugoma, kiliambulia magunia 26 ndipo wananchi walipokuja juu na kugundua
wizi huo. 
Mkuu wa Wilaya hiyo, Joshua Mirumbe, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kudai kuwa, tayari amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri amsimamishe kazi, Katikizu
kwa kosa hilo.
“Huyo Ofisa Mtendaji habari zake ninazo, aliwahi kuiba na kuuza mitumbwi 20
iliyokamatwa katika uvuvi haramu hivyo kutokana 
na tukio hili, nimeagiza Mkurugenzi amsimamishe kazi kuanzia 
leo (jana) na ashitakiwe kwa wizi,” alisema Mirumbe.
Alisema viongozi wa namna hiyo hawafahi kuendelea kuongoza na wanaitia doa
Serikali hivyo hawana budi kuondoka wabaki viongozi waaminifu na waadilifu
watakaowaletea wananchi maendeleo. 
“Siko tayari kuona viongozi wezi, wabadhilifu na wababaishaji wakiendelea
kuwanyonya wananchi kwa kuwaibia, kama wapo wajiondoe kabla sijawafikia,
nitaanza na huyo Ofisa Mtendaji 
ili iwe mfano kwa wengine,” alisema.
Majira lilipomtafuta, Katikuzu na kumuuliza juu ya tuhuma hizo alidai madai
hayo ni uzushi uzushi na hakuna wizi wowote aliofanya bali yeye ni miongoni mwa
Watendaji waadilifu wilayani humo wanaoaminiwa kiutendaji na. Mirumbe.
Juma Mtanda
 
Source: Marayetu Blog

No comments:

Post a Comment