Hivi karibuni nilisafiri kwa ajili ya Likizo ya mwaka katika Wilaya za Bunda na Musoma Vijijini.
Chakula kikuu katika wilaya hizi kiasili imekuwa Muhogo na Mahindi, lakini kwa miaka ya karibuni zao la Mhogo lilikumbwa na ugonjwa wa Cassava Meal Bug na kusababisha zao la muhogo kutoweka kwa asilimia kubwa.
Hali hiyo inajitokeza sasa kwenye zao la Mahindi, na kwa kuwa Wakulima wa mikoa ya kanda hii ya ziwa hawana utamaduni wa kutumia viuatilifu kwenye mazao ya chakula, inaelekea hali ya upatikanaji wa Chakula itakuwa ngumu.
Wakulima waliowahi kulima mahindi mwezi wa Tisa na wa Kumi ndio pekee waliofanikiwa kupata mavuno. Waliolima kuanzia Novemba na kuendelea, kwa maeneo yote niliyopitia Mahindi yameshambuliwa na wadudu na hakuna matarijio kabisa ya kuvuna.
Wakulima pekee wenye matarajio ya kupata walau chakula kwa musimu huu ni wale walioweza kulima Mtama na Uwele.
Maofisa Ugani na Serikali bila ya shaka wataliona tatizo hili na kulitafutia ufumbuzi wa kudumu.
No comments:
Post a Comment