Total Pageviews

Sunday, April 23, 2017

BACK TO MTWARA AFTER 34 YRS

Back in December,1983
Blogger, nikiwa Askari kijana R 3747aliyemaliza Mafunzo ya JKT, Oparesheni Safisha, Nachingwea wakati nikirejea kituo cha kazi Bagamoyo nilibahatika kupitia Mtwara. Mji uliokuwa ukifikika kwa shida kutokana na taabu ya usafiri.
Miezi michache kabla ya hapa, Mwanasheria Nyachiriga ndiyo alikuwa ameingia mjini hapa kuanza maisha kama Afisa wa Ardhi wa Upimaji.
Nilikaa Mtwara kwa takribani wiki moja hadi tulipopata usafiri wa kurejea Dar kwa MV Mapinduzi.
Pamoja na mipango mingi ya kutaka kutembelea Mtwara, haikuwezekana.
Lakini hatimae, baada ya miaka 34 kupita ninafanikiwa kurejea Mtwara kwa ajili ya kuja kuhani musiba wa mama yetu.
Ni safari ya kusisimua, yenye kuvuta Kumbukumbu za zamani.
Blogger, pamoja na uzee wa sasa najiandaa na Kamera mkononi kwa ajili ya kukuachia kumbukumbu.
Ni siku ya Ijumaa Kuu

 Temeke Sudan, mapema asubuhi kwa ajili ya kupata Tiketi za Safari.
Pamoja safarini ni wadau Baruku "Honda" na Msalya "Tall"
 Tunaabiri na Millenium Coach ya kuondoka Dar saa Tatu.
 
 
NANGURUKURU
Stop Over yetu, kwa ajili ya uchimbaji dawa na "Breakfast ya mchana"
Pahala maarufu kwa vitoweo vya samaki.........
Blogger Kamera mkononi
 
 
LINDI
Second stop Over.
Niliwahi kupita Lindi zamani.
Juni 1983, tukiwa on transit kuhamishwa Kambi za JKT nikitokea Ruvu kwenda Nachingwea.
Ni safari isiyosahaulika ya miaka hiyo,
Safari ya siku tatu kwa MV Lindi.
Lakini leo ni safari ya Masaa Manane na Millenium Coach
 Lindi bus Stand
 
Ming'oko
Bidhaa maarufu kusini.
 
Hatimae baada ya takribani masaa kumi njiani tunawasili Mtwara.
Mtwara ni moja ya miji jua linazama mapema.
Mnara wa Uhuru, unaobeba sasa pia nembo ya Ukimwi na Mnara wa mashujaa, Tanu Road ni Vitambulisho muhimu vya mji huu wa Mtwara ulio kusini mwa nchi yetu.

No comments:

Post a Comment