March 16th, 2013 by Stella
Mwaikusa
Shule ya msingi ya Kinyambwiga
iliyopo kata ya Guta wilayani Bunda, inakabiliwa na uhaba wa madarasa na
madawati hali inayowapa wakati mgumu walimu na wanafunzi wa shule hiyo.
Kutokana na hali hiyo wanafunzi
wanalazimika kusomea chini ya miti huku wakikalia mawe na wengine wakikalia
mabanzi.
Mwalimu wa somo la stadi za kazi
darasa la sita B Kastori Mng’ong’o, anasema inamwia vigumu kufundishia chini ya
mti kwani watoto wanakosa utulivu na kuiita hali hiyo kwamba ni “msingi
mbaya kwa wanafunzi hao.”
Anasema wanafunzi wakiwa hapo nje
wamekuwa wakipoteza utulivu pale wanapoona mtu au gari linapita, na
kuondoa usikivu ambao ni mhimu sana kwa mtoto katika kujifunza.
Mwanafunzi wa darasa la sita Ubwe
Juma anasama inampa wakati mgumu kupangilia mwandiko wake, kwani mara nyingi
mawe anayoandikia hutingishika na wakati mwingine kudondoka kabisa.
Anasema pamoja na mwandiko kuwa
mbaya bado suala la usafi kwao ni gumu kwani mawe hayo yana vumbi na kujikuta
wakisoma huku wakiwa wamechafuka.
Mwalimu mkuu wa shule ya Kinyambwiga
Leornald Mukama anasema kumekuwa na mipango ya kujenga madarasa lakini bado
wanasubiri kwani yeye hana uwezo wa kufanya lolote.
Source: Jamii Forums
No comments:
Post a Comment