Total Pageviews

Monday, March 28, 2011

BAGAMOYO VEKESHENI

Jana jumapili, nikawa nimetakiwa kwenda Mjini Bagamoyo kikazi.

Ikabidi kumuunganisha na Mzee CK, yeye aliplani kwenda kumusalimia mchambwe Mr Hadji.

Manyori na CK nao wakadandia trip.

Blogger kama kawaida akaweka pembeni Olympus na Kinokia

Njiani CK Jr akawa akivutiwa na taswira mbali mbali na kuweka kumbukumbu..... Mojawapo ya Taswira, ni Total Mlimani City. Kazi moja safi sana ya kampuni yetu ya Delmonte Breki ya kwanza ikawa maeneo ya Soko jipya kwa ajili ya breki fasti Nikapata bahati ya kukutana na Bwana Kitwana, jirani yangu miaka ile ya late 1980 na early 1990 na baadae office mate pale BADECO BEACH HOTEL
Breki fasti kila mtu kwa chaguo lake

chai ya mkandaa na chapati..
Supu ya kolekole................
Supu ya mbuzi...................
Tukapata nafasi ya kupatembelea hapa, Nyumba niliyoanzia maisha ya kupanga Bagamoyo Oktoba 1982. jirani na kwa Mzee Sudi, maarufu sana Bagamoyo enzi hizo akimiliki mabasi kadhaa ya abiria Dar - Bagamoyo
Tukapitia Customs ya miaka hiyo kuangalia bahari..........
na baadae kuelekea Makumbusho kule misheni, maarufu kama mantep

Pametulia...
Wadau wakashangaa shangaa humo ndani baada ya kuwa tumelipia buku na nusu kwa kichwa ili kupata ruksa ya kuingia kushangaa............

a nice place to visit
Kasiki, made in Austria in 1870
Mbuyu uliotumiwa na Nurse kufungia punda wake, karibu miaka 100 iliyopita.

Mnyororo ungalipo ingawa unazidi kumezwa na mmbuyu.

Hapa napo nikapata nafasi ya kukutana na Bi Selina.

Wakati naanza kazi Bagamoyo huyu ndiyo alikuwa Sekeretari wetu wa Idara ya Ushirika na maendeleo ya jamii, chini ya Mzee Mkodo na baadae Mujos


Kosa la Blogger, Olympus haikuwa na chaji ya kutosha..........

ikabidi Kinokia kichukue nafasi kupata taswira ya hili kanisa la awali kabisa ukanda huu wa Afrika Mashariki miaka zaidi ya 100 iliyopita
Hapa ndipo mwili wa Bw. Livingstone ulipolazwa wakati wa kusafirishwa toka Kigoma kupelekwa kwao.
mtaani nako Kinokia hakikukosa taswira.....

muda ulikuwa mchache, tulipaswa kugeuka mapema ili kuwahi mkutano wa wana ndugu uliokuwa unafanyika Kipunguni kwa Bw Eddyson

No comments:

Post a Comment