Total Pageviews

Monday, December 11, 2017

WAIJUA KABILA YA VADOMA

 Kabila ya Wa Vadoma, hujulikana pia kama Dema. Hupatikana Mkoa wa Kanyemba, Kaskazini mwa Zimbabwe kwenye wilaya za Urungwe na Sipolilo.
 Watu wa kabila hili wanakabiliwa na hali ya maumbile ijulikanayo kama "Etrodactyly".
Tatizo hili pia hujulikana kama "Miguu ya Mbuni" na huweza kuathiri Mikono na Miguu.Vidole vya kati hukosekana, na vile vya pembeni hukunjika ndani.
 Tatizo la Miguu ya Mbuni hutokea 1 kati ya 90, Lakini kwa Wa Dema ni kubwa kwa sababu wao wanasisitiza kuoana wao kwa wao tu.
Wa Dema ni waumini wa madhehebu yao ya kiasili au kanisa la Waadiventista Wasabato.

No comments:

Post a Comment