Darasa la Awali kabisa 1949 lilijengwa hapa
Karibuni nimepenyezwa wazo na Wadau wa Elimu, Ni
wadau wa Elimu waliowahi kusoma shule ya msingi Namalebe iliyopo kata ya Kibara , Jimbo la Mwibara. Shule
ya Msingi Namalebe ilianzishwa yapata miongo saba iliyopita, Ilianza
mwaka 1949 ,hivyo panapo majaliwa itakapofika 2019 shule hii itakuwa inatimiza
miaka 70 ya kutoa Elimu.
Wadau wa Elimu wanaona ni wakati wa Wasomi wote waliopitia
hapo kurudisha kidogo kama ishara ya shukrani .Wadau wanafikiria ni vyema kuwa
na Sherehe za Platinum Jubilee kutafakali ilikotaka Namalebe, ilipo na inapoelekea. Namalebe
ndiyo shule ya mwanzo kabisa katika jimbo la Mwibara, lakini pamoja na
kukaribia miaka miongo saba, bado iko nyuma sana kulinganisha na shule
zilizokuja baadae.
Binafsi kama mdau, tena
mwenye rekodi ya kuwa kati ya wadau waliosoma kwa miaka mingi Namalebe nawiwa,
Na hata nilipotakiwa na Wadau wa Elimu wa Namalebe
kuweka makala mtandaoni ya uchokozi wa kutafutana wote waliopitia shule ya
msingi Namalebe, sikusita…………..
Lakini baadae
nimejikuta njia panda,sijui pa kuanzia. Tutafurahi sana kupata habari zako mdau
wa Elimu wa Namalebe. Tafadhali tutumie mawasiliano yako, au namna tunavyoweza
kukufikia au mapendekezo yako yoyote. Nyumbani Namalebe na Nakatuba Bwana
Tungura Misana Mkhoi ( Class of 1963 ) Na Goodluck M. Ngalya ( 0629 417631 )
wako tayari kupokea habari uliyonayo kuhusu Namalebe.
Bw Nyande Misana Mkhoi ( 0713 730 232 ) Kanda ya
kaskazini anapokea habari yako mdau kama ilivyvo kwa Mwl Msataafu Belly Msalya
( 0759 390 575 ) aliyeko Bunda. Tuna Mratibu Kanda ya Kusini Bw. Bright ( 0717
404 885 ) na Dar Es Salaam tunao Bw
Machele ( 0754 824375 ) na mimi mchokozi wa makala hii kwenye namba 0713 236 990.
Tupe habari yako, maoni
na ushauri kusudi tujipange vipi kwa
ajili ya Platinum Jubilee ya Namalebe mwishoni mwa 2019.
Mr Ernest Munubhi Magoti, Early Schoolers 1949
NAMALEBE
1949
Kiguu na njia kutafuta
habari za Namalebe.
Mabhui Merafulu, Majita.
Ndipo makazi ya mstaafu na sasa mkulima Bw.
Ernest Mnubhi Magoti. Mzee Magoti anaikumbuka Namalebe 1949 ilipoanza.
Anakumbuka jinsi wajenzi wakivuna miti Kurwirwi ( Nyasuruli ) kwa ajili ya
ujenzi wa shule. Wakati huo wakikaa kwa Mzee Malekela Nyachemo. Mwanafunzi
mwenzie ni Binti wa Malekela, Bi Nyabwire, sasa mjane wa Marehemu Yoel Masano
makazi yao Namuhula.
Marco Riganya House Late 1960
Sylivester and Martin resided here.
Mwl Eliab Mkama residence
Makaranga Ndimila Residence
WALIMU
Siku zinaenda mbio,
Namalebe inasonga. Walimu wengi wamepita hapa. Si rahisi kuwakumbuka wote kwa
mara moja.
Sospiter Malegesi
alipita hapa, Marco Riganya Mwalimu Mkuu kwa wakati wake, maarufu kwa Scooter
yake kijijijni, lakini nadra kukutana na wanafunzi maana wakiisikia kabla
mtaani. Siku moja moja akiingia pembezoniya kijiji kwa mawindo ya Kanga na
Rifle yake.
Faustine Makaranga
Ndimila, Specialist kwa wanafunzi wanaoanza. Kama unakumbuka vizuri hupokelewi
mpaka mkono wa upande mmoja umeshika sikio la upande wa pili kwa kupitia
kichwani. Mzee huyu ndiyo baba yao na Marehemu Godfrey na Albert na Binti Felista
ambae mara ya mwisho tulikutana JKT RUVU, Mwl Makaranga nasikia makazi yake yako
Bunda kwa sasa, Mwl Haruni Pamba, Seif Mkome maarufu kwa hesabu ya kichwa. Mwl
Chibiriti , mtoto wa mjini. Young and ambition Teachers Sylivester and Martin.
Sylivester alikuja baadae kuwa mume wa mwanafunzi Penina Malegesi. Bahati
ilikua upande wake, sheria ya miaka 30 ilikua haijaanza.
Mwalimu Mkuu wa enzi
zetu Marehemu Eliabu Mkama The Linguistic Teacher na kitabu chake kisichochuja
“Common mistakes in English” pamoja na Mkewe Mwl Damali Mkama mbobezi wa Hesabu
na Maarifa ya nyumbani. Not the last Mzee wetu Alphaxard Maleka Matekere akirejea nyumbani Namalebe miaka ya katikati ya 70
bila ya shaka akijiandaa kustaafu baada ya kulitumikia taifa miaka mingi sehemu
mbalimbali.
Ujio wa Mzee Maleka
ukiwatia kiwewe wanafunzi kuwa ni Mwl mkali. Kumbe hofu tu, hakua tena na mkono
wa kuchapa viboko, akawa Mwl mshauri kwa walimu na wanafunzi wote, wanae Marehemu
Lawi na Jamhuri ndio wakapata nafasi ya
kuja kumalizia elimu yao ya msingi
Namalebe. Jamhuri a.k.a Maradona ndie
amebakia icon ya Boma la Mzee Maleka kijijini kwetu.
NAMALEBE
NA STD V
Baada ya miaka 22,
Hatimae Namalebe inapata darasa lake la tano la kwanza. Kwa furaha hiyo wanafunzi wote waliofanya mtihani wa kumaliza
drasa la nne wanachaguliwa kuendelea na darasa la tano. Tukiwakumbuka wadada
hawa ni pamoja na Akisa Samwel Ngalya, Sherida Mgeta, Penina Manyama, Chausiku
Nyamwaga, Dorika Muyemba na Penina Maregesi aliye kuja baadae kuwa mke wa Mwl
Sylivester. Kwa mara ya kwanza pia Namalebe ikapata wanafunzi kutoka Mkoko na
Igundu. Wanafunzi Nicodemus na Mtaka kwa uchache, waliojinasibu kutokea
“Bhughuma Ku Mwandu”.
FIRST LY CLASS OF 1973
Darasa la kwanza
kumaliza la saba linatimia 1973. Sina kumbukumbu njema ya waliochaguliwa kwenda
kidato cha kwanza, Lakini bila ya shaka watakua ni Robinson na Marehemu Godfrey
Ndimila.
Mimi binafsi ilibidi
nisubirie LY ya 1975 tulipochaguliwa pamoja na Marehemu Engineer Naftali
Mjinja.
Mr Machele,
One among the first Class Seven Graduates 1973
Current Administration Building
WANAFUNZI
Kwa umri wa shule ya
Msingi Namalebe, kwa wastani wa wanafunzi 45 kila mwaka, kwa kufikia mwaka wa Jubilee
2019, Basi bila ya shaka wanafuni zaidi ya elfu tatu watakua wamepitia
hapa. Si rahisi kuwakumbuka na kuwapata wote, wengine wametangulia mbele ya
haki,wapumzike kwa amani .wengine wana majukumu mazito ya kuitumikia nchi
,lakini pia wapo waliobakia vijijini mwao hawana mbele wala nyuma .Lakini kwa
makala yangu hii, nawakusudia wote. Ulipitia shule ya msingi Namalebe, ulivuna
nini Namalebe japo kidogo. Upo tayari kuirudishia Namalebe kidogo kutoka kidogo ulichopata kwayo?
Tujipange kwa ajili ya
Jubilee ya Namalebe ya miaka 70.
Ernest Magoti, Nyabhwire
Malekela Yoel, Class of 1949, Tungura Missana Mkhoi , Class of 1963. Na kizazi
cha uhuru hadi sasa.
Finias Machele, Chanika
Dar Es Salaam , Benjamin Masatu, Dar Es Salaam, Nyande Misana Mkhoi, Arusha.
Rusasa Matekere, Mirobo Daudi, Juma Daudi, Lusoti Chiganga, Kalega Mgeta,
Shabani na Fatuma mliofanya tukajua siku za mapumziko za watu wa imani ya
kiislamu , Ndaro Mnaga , Goodluck M. Ngalya a.k.a Chadema, Daudi Mkani,
Sumbawanga, John Mkani , Manyonyi Alex Kasoli Zakayo Chiganga na Dada zetu
niliwataja awali pamoja na wengi wengineo. Kaka Mfungo Afisa Ugani, Tarime
mwanariadha mahiri, ukitoa ushauri wa matumizi ya glucose miaka hiyo.
Kama kwenye njia yako
ya Elimu ulipitia Namalebe, wewe ni mdau wetu. Tutafutane.
Makala hii itawekwa
mtandaoni kwa Hisani ya Blog ya Msalya MyFamily, www.msalya.blogspot.com,
lakini pia itanakiliwa kwenye Ukurasa wa Facebook wa Billy K Msalya.
Wadau wetu tunaombeni m
”Share” kadri mtakavyoweza kwa ajili
ya kufikisha ujumbe kwa wadau wengi wa Namalebe wa kizazi cha zamani na cha
sasa cha dotcom.
#Toward Namalebe
Platnum Jubilee 2019
# Tukumbuke tulikotoka
#Shule yangu Namalebe
No comments:
Post a Comment