Msimbazi Centre, Jumamosi alasiri.
LUKA 10: 25-37
25Baadaye mwanasheria mmoja alisimama, akamwuliza akitaka kumtega, “Mwalimu, nifanye nini ili nipate uhai wa milele?” 26Yeye akamwuliza, “Imeandikwa nini katika sheria? Unaelewaje?” 27Akamjibu,
“Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa
nguvu zako zote na kwa akili yako yote. Na, mpende jirani yako kama
unavyojipenda mwenyewe.” 28Yesu akamwambia, “Vema! Fanya hivyo, nawe utaishi.” 29Lakini yeye akitaka kujihakikishia kuwa mwema akamwuliza Yesu, “Na jirani yangu ni nani?” 30Yesu
akamjibu, “Mtu mmoja alikuwa anashuka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko.
Alipokuwa njiani, alivamiwa na majambazi, wakamnyanganya mali yake na
kumpiga, wakamwacha amelala pale nusu mfu. 31Kumbe, kuhani mmoja akawa anapita barabara ileile, akamwona, akapita kando. 32Hali kadhalika na Mlawi mmoja, alipofika mahali hapo akamwona, akapita kando. 33Lakini Msamaria mmoja aliyekuwa anasafiri, alifika pale yule mtu alipokuwa, naye alipomwona, alimwonea huruma. 34Akamwendea,
akamtibu majeraha yake kwa kumtia mafuta na divai na kuyafunga; halafu
akampandisha juu ya punda wake, akampeleka katika nyumba moja ya wageni
akamwuguza. 35Kesho
yake akatoa fedha dinari mbili akampa yule mwenye nyumba, akamwambia,
‘Mwuguze mtu huyu; na chochote utakachotumia zaidi, nitakulipa
nitakaporudi.’” 36Kisha Yesu akauliza, “Kati ya hao watatu, ni yupi aliyeonesha kuwa jirani yake yule aliyevamiwa na majambazi?” 37Yule mwalimu wa sheria akamjibu, “Ni yule aliyemwonea huruma.” Yesu akamwambia, “Nenda ukafanye vivyo hivyo.”
No comments:
Post a Comment