Total Pageviews

Friday, September 18, 2015

32 YEARS IN THE MTWARA, AND STILL.................

Pamoja na kwamba Mzee wa Halmashauri  kwa sasa ni Mwanasheria anaetambuliwa kisheria na serikali, ametokea mbali. Mwanzoni mwa mwaka 1983 alipelekwa kuanza kazi Mtwara kama Land Surveyor. Anakumbuka kuwa baada ya kuhitimu pale Chuo cha Ardhi yeye pamoja na wenzie watatu walipangiwa kwenda kufanya kazi kusini.
Ndani ya kipindi kifupi wenzie wote walikuwa wameondoka Mtwara kila mmoja kwa sababu na mipango yake, lakini Mzee wa Halmashauri ameendelea kubakia kule hadi leo..........
Takribani miaka 32.
Majuzi ame "share" nasi picha za makazi mbalimbali aliyowahi kuishi............
Tuungane nae.
 Chumba chake cha kwanza kupanga ilikuwa hapa kwa Mzee Omari Bakari(pichani) tarehe 18 May 1983. Eneo la Chikongola, Zambia Road
Chumba hiki cha uwani kingalipo hadi leo.

October 1983 hadi 1991, Makazi yalikuwa chumba hiki cha uani. Nyumba sasa ina mmiliki mpya.
Kuna historia kubwa hapa, kwani hapa ndipo alipozaliwa Lulu na Neema.
Wageni wa kukumbukwa hapa ni Beria (1984) na Msibha Mjengwa.
Hii nyumba kama inavyoonekana maeneo ya Raha Leo, Mtaa wa Uhuru.

1991 hadi 1995, Makazi yalihamia maeneo ya Kiyangu, Nyumba ya aliyepata kuwa Mbunge Mh Zalari (Pichani na mkewe).
Na hapa ndipo alipozaliwa Rebeca Nyamweya.
Shukurani kwa Manispaa ya Mtwara Mikindani iliyokuwa ikilipia kodi yote ya nyumba hii nzima.
 Makazi binafsi, banda la nyuma kuanzia 1995
Nyumba kubwa1998, Maeneo ya Ligula "A" low density plots. Ni karibu na Hospital ya mkoa na Police lines.
 FOCONA Head Quarter Mitaa ya Shangani.


Kati ya July 1983 hadi Mwishoni mwa mwaka huo Makazi yalikuwa Mitaa ya Chikongola msikitini kwenye nyumba hii. Ni hapa alipofikia pia Blogger wakati wa kumaliza Mafunzo ya mwaka mmoja ya Jeshi la Kujenga Taifa, kambi ya Nachingwea (Oparesheni Safisha).
Lakini pia akipita mara kwa mara Marehemu Mwl Lawi Mareka Matekele wakati akisoma chuo cha Ualimu Nachingwea.

No comments:

Post a Comment