Total Pageviews

Thursday, September 4, 2014

KILA KAZI NA CHANGAMOTO ZAKE

Kila kazi ina ugumu wake,
Kondakta wa daladala pale gari yake inapoharibika inahitajika umakini mkubwa.
Abiria wote wanadai kurudishiwa nauli, hata wale waliokuwa wamepungukiwa wanahitaji full.
Waliokuwa washuke kituo kinachofuta wanahitaji full.
Usipotahadhari wapita njia nao watadai nauli full.
Mwisho wa yote unakuta pamoja na panda shuka ya abiria njiani, umerudisha kila kitu bila kubakiwa na senti, pengine bado ukidaiwa.
Naam, ni changamoto tu,
Na ni kwa kila aina ya kazi.
Kawawa Road, Jumanne

No comments:

Post a Comment