Total Pageviews

Thursday, June 16, 2016

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA

 Kila mwaka tarehe 16/6 watoto wote Afrika huadhimisha siku ya mtoto wa afrika ikiwa ni Sehemu ya kumbukumbu ya kuwakumbuka watoto wenzetu waliouawa kikatiri huko Soweto Afrika kusini walipokuwa wakiandamana kwa amani kupinga utawala wa kibaguzi uliokuwa ukiendeshwa na makaburu. Katika siku hii watoto hutumia fursa hii kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya masuala mbalimbali yanayohusu malezi, makuzi, matunzo ulinzi na usalama wa watoto.

 Uamuzi wa kihistoria ulifikiwa tarehe 20 Novemba 1989 pale viongozi wa dunia waliporidhia Mkataba kuhusu Haki za Mtoto katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Tangu kuridhia kwake miaka 20 iliyopita , Mkataba huu umevunja rekodi kwa kuwa mkataba wa haki za binadamu iliowahi kuridhiwa na mataifa mengi kuliko yote katika historia. Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi za mwanzo kabisa zilizoridhia Mkataba huu katika mwaka 1990 na kwa kufanya hivyo ikawa imetambua rasmi kwamba watoto wote wanayo haki ya kuishi na kukua, kupatiwa ulinzi dhidi ya vurugu, matendo mabaya na unyanyasaji, kuheshimiwa kwa mawazo yao na kuzingatiwa kwa maslahi yao katika maamuzi yote yanayohusu ustawi wao.


No comments:

Post a Comment