Final Lap ya vacation yangu inaanza Jumatatu 24/10 Alfajiri Mwanza. Tofauti na wakati wa safari ya kuja Nakatuba, On wheel nabakia mimi pekee, no Co Driver.
Kuna Mabadiliko ya abiria pia.
Tuongozana na Mzee CK, Mama Tereza, Beria, Joshua na Nyamtakama
Majira ya saa tano tunaingia Singida Town, abiria wangu inaelekea wako hoi kwa safari. Lakini tunajipa moyo, milima ya kutisha tumekwisha ipita
Stop Over Singida inatukutanisha na Dada Pendo Yoweli.
Baada ya miaka mingi namna hiyo tunapata nafasi ya kupeana kilichojili tokea wakati huo.

Baada ya miaka mingi namna hiyo tunapata nafasi ya kupeana kilichojili tokea wakati huo.
Chai, Chapati na maandazi
Soda kupooza koo na vijinyama choma
Kilometa 35 kabla ya Manyoni pancha ingine, hatuna spare tyre.


Baada ya hapo safari inaendelea, kilometa 45 kabla ya Dodoma tunajikuta hatuna mafuta.
Baada ya mahangaiko ya hapa na pale tunafanikiwa kupata Mafuta na kuingia Dom usiku
Asubuhi Dom ninapata hizi Taswira mbili
Ndani ya Kongwa Ranchi tunapata pancha ingine. Tuweka the only spare tuliyokuwa nayo
Duh, misukosuko mmeipata. lakini bora mmefika slama. Mungu ashukuriwe kwa yote.
ReplyDeleteasante Uncle kwa kumbukumbu hizi.
Poleni, ni zamani ila mlihangaika sana!
ReplyDelete