Jana alasiri
Thursday, June 25, 2015
Tuesday, June 23, 2015
ANA KWA ANA NA JK
Hatimae baada ya takribani miezi minne toka azaliwe, Joshua Joel Joshua Kaitila "JK" alifika kumwona Babu.
Kinyerezi kwetu, Jumapili
Kinyerezi kwetu, Jumapili
KICHEKO KINAREJEA
Yote ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu,
kwani maisha yanapaswa kuendelea.
Tunashukuru taratibu simanzi inatoweka, na Kicheko kinatamalaki kwenye nyumba.
Nyumbani kwa Jackson, Jumapili
kwani maisha yanapaswa kuendelea.
Tunashukuru taratibu simanzi inatoweka, na Kicheko kinatamalaki kwenye nyumba.
Nyumbani kwa Jackson, Jumapili
Tuesday, June 16, 2015
Monday, June 15, 2015
MICHANGO YA RAMBIRAMBI
Kinyerezi, jana jioni.
Wanandugu jana tulikutanika nyumbani kwa Marehemu Jackson,
pamoja na kumfariji Happy (Mama Carol) tulitumia fursa hiyo
kuwasilisha michango yetu ya rambirambi ambayo imekwisha patikana.
Michango inaendelea kukusanywa.

Saturday, June 13, 2015
ALMANUSURA NYINGINE
Ahsante Mungu,
Tumenusurika na ajali asubuhi hii, Tairi ya nyuma kushoto ilichomoka.
Ukiangalia kwa makini mstari mweupe, ni usawa nyuma kidogo ya Mwendesha pikipiki.
Nimefanikiwa kulithibiti gari na kusimama pembeni. Na bahati nzuri nuts zote zikapatikana tukafunga na kuendelea na safari.
CFAO Motors (DT Dobie), Nyerere Road maarufu kama Karakana
Leo asubuhi

Monday, June 8, 2015
Friday, June 5, 2015
Thursday, June 4, 2015
HII NDIO AJALI ILIYOMUUA MPENDWA WETU JACKSON
Mtu mmoja amefariki dunia papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa baada bas la kampuni ya Dar Lux likitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza kugongana uso kwa uso na mistubishi fuso katika eneo la njia panda ya Berega wilaya ya Gairo barabara kuu ya Morogoro Dodoma.
Kwa mujibu wa mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Bonifas mbao
amesema aliye fariki ni abiria aliye kuwa kwenye basi na chanzo cha
ajali ni mwendo kasi wa dereva wa fuso alitaka kulipita gari jingine
bila tahadhari na kusababisha ajali ya uso kwa uso.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema chanzo cha ajali ni uzembe wa
dereva wa fuso ambapo gari ilimshinda kutokana na utelezi katika eneo la
Berega na kusababisha ajali hiyo.
Wednesday, June 3, 2015
UTUMIAJI FURSA
Kuitumia Fursa,
Umeajiriwa Hospitali ya Muhimbili, kitengo chako Wadi ya wazazi.
Vitoto vinazaliwa kila siku, vinahitaji vijinguo kama vile visweta n.k.
Mama zao hawajawa na nguvu za kutosha kwenda kuwatafutia,
Hiyo ni fursa kwa Mkunga huyu....................
Duka la nguo za watoto litembealo mawadini.

BABA NA MAMA WAWILI
Baba na Mama wawili,
Muhimbili National Hospital on Sunday.
Mama wawili was discharged from Hospital yesterday afternoon.
HERE RESTS THE TWINS
Tarehe 28 May 2015 tukimshukuru Mungu na kumtukuza kwa mapenzi yake kwa kuwajalia Makubhi na mchumba wake watoto mapacha wa kiume, pamoja na kuzaliwa "Njiti" ilikuwa ni jambo lenye heri na baraka.
Pia tarehe hiyo hiyo akitujalia mtoto mwingine wa kiume kupitia kwa binti yetu Penina wa Nyang'oko, pamoja na kupatikana kwa njia ya upasuaji tunazidi kumtukuza Mwenyezi Mungu.
Hata hivyo kwa wingi wa rehema zake, na Mapenzi yake Mwenyezi Mungu aliamua tena kuwaita tena mapacha wake.
Doto (29.05.2015) baaada ya kuwa amepata matatizo ya upumuaji yaliyosababisha wakati mwingine kuwekwa kwenye mashine ya hewa.
na Kulwa (31.05.2015) baada ya matatizo ya kujaa gesi tumboni.
NI BWANA ALITOA, NA NI BWANA ALITWAA
JINA LAKE LIZIDI KUHUMIDIWA
KWAHERI JACK
Kwaheri Jackson Kaigi Marogo,
Ni vigumu kuamini, lakini ni vyema kukubali kuwa umetangulia....
Kwangu mimi hukuwa Mkwe tu, Ulikuwa ni Rafiki wa dhati, ndugu wa damu......
Bado naona kama ndoto tulivyokaa wote pale Samunge ukinipa ratiba yako ya safari,
Ndoto zako...............
Hata baadae wakati nikiangalia mpira pale Flamingo, sms yako iliponifikia, nikakupigia tukaongea tena.
Kuja kuambiwa baadae kuwa hauko nasi tena, ni jambo linaloumiza.
Tangulia, ni njia ya kila mja wake Mwenyezi Mungu.
Mapenzi yake Mwenyezi Mungu yatimizwe, Ni yeye alitoa na yeye ametwaa kilicho chake.

KWAHERI
JACKSON KAIGI MAROGO
08.03.1962 - 31.05.2015