Thursday, June 4, 2015

HII NDIO AJALI ILIYOMUUA MPENDWA WETU JACKSON


Mtu mmoja amefariki dunia papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa baada bas la kampuni ya Dar Lux likitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza kugongana uso kwa uso na mistubishi fuso katika eneo la njia panda ya Berega wilaya ya Gairo barabara kuu ya Morogoro Dodoma.
Kwa mujibu wa mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Bonifas mbao amesema aliye fariki ni abiria aliye kuwa kwenye basi na chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa dereva wa fuso alitaka kulipita gari jingine bila tahadhari na kusababisha ajali ya uso kwa uso.
 
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa fuso ambapo gari ilimshinda kutokana na utelezi katika eneo la Berega na kusababisha ajali hiyo.
 
SOURCE:

1 comment: