Wednesday, June 3, 2015

KWAHERI JACK

Kwaheri Jackson Kaigi Marogo,
Ni vigumu kuamini, lakini ni vyema kukubali kuwa umetangulia....
Kwangu mimi hukuwa Mkwe tu, Ulikuwa ni Rafiki wa dhati, ndugu wa damu......
Bado naona kama ndoto tulivyokaa wote pale Samunge ukinipa ratiba yako ya safari,
Ndoto zako...............
Hata baadae wakati nikiangalia mpira pale Flamingo, sms yako iliponifikia, nikakupigia tukaongea tena.
Kuja kuambiwa baadae kuwa hauko nasi tena, ni jambo linaloumiza.
Tangulia, ni njia ya kila mja wake Mwenyezi Mungu.
Mapenzi yake Mwenyezi Mungu yatimizwe, Ni yeye alitoa na yeye ametwaa kilicho chake.
 KWAHERI
JACKSON KAIGI MAROGO
08.03.1962 - 31.05.2015

1 comment:

  1. Mr.Kaigi amelala
    Tuwe tayari, maana kifo ni hakika
    MUNGU awape faraja familia

    ReplyDelete