Wednesday, June 3, 2015

HERE RESTS THE TWINS

Hakika Mungu hutenda kwa mapenzi yake,
Tarehe 28 May 2015 tukimshukuru Mungu na kumtukuza kwa mapenzi yake kwa kuwajalia Makubhi na mchumba wake watoto mapacha wa kiume, pamoja na kuzaliwa "Njiti" ilikuwa ni jambo lenye heri na baraka.
Pia tarehe hiyo hiyo akitujalia mtoto mwingine wa kiume kupitia kwa binti yetu Penina wa Nyang'oko, pamoja na kupatikana kwa njia ya upasuaji tunazidi kumtukuza Mwenyezi Mungu.
Hata hivyo kwa wingi wa rehema zake,  na Mapenzi yake Mwenyezi Mungu aliamua tena kuwaita tena mapacha wake.
Doto (29.05.2015) baaada ya kuwa amepata matatizo ya upumuaji yaliyosababisha wakati mwingine kuwekwa kwenye mashine ya hewa.
na Kulwa (31.05.2015) baada ya matatizo ya kujaa gesi tumboni.

NI BWANA ALITOA, NA NI BWANA ALITWAA
JINA LAKE LIZIDI KUHUMIDIWA

No comments:

Post a Comment