Total Pageviews

Monday, July 30, 2012

AHSANTE YANGA AFRICA

Ahsante Yanga Africa
Hakika kwa kutwa Kombe la Kagame mmetutoa kimasomaso na tunaweza kutembea kifua mbele.
Hata zile jezi zetu ambazo muda mrefu zimekaa masandukuni, juzi, jana, leo kesho na hata mtondogoo zitavalika.

HOMEWORK TYME

CK
Wahida
East Africa inavyoonwa na CK
 East Africa inavyoonwa na Wahida
Minoo

 

BREKINGI NUWZ - SERIKALI HAITUJALI

Wanafunzi wa shule ya msingi wamepita hapa wakiandamana muda si mrefu kuelekea kwa Mkuu wa kaya ya Bongo, Mh Meki Sadick.
Wanasema Serikali haiwajali.
Haiwajali nini, hatujajua...............
Lakini inaelekea ni salamu kutokana na mgomo wa Walimu uliotangazwa inji nzima kuanzia leo.
Sisi macho na masikio kwenye source nyingine za habari.
Tungoje na tusikie.

Friday, July 27, 2012

MWANAMME HUSIFIWA KWA KAZI

Ama kwa hakika mwanamme unapaswa kusifiwa kwa kuchapa kazi, ili kuitunza vema familia na wategemezi wengine.
Pichani, Mwanamme akiwa kazini jana mitaa ya Msimbazi, Kawawa Road.
Kwa uchache mzigo unakadiriwa siyo chini ya Kgs 500 (Nusu Tani)

Wednesday, July 25, 2012

PODA DAWA YA KUWASHWA!!!!!!!!!!!!!

Leo katika hazina ya dawa ninazozijua nimeongeza moja.
Kwamba Poda ni dawa ya muwasho wa ngozi/mwili

ITS TV SHOW TIME

Rev Moses Kulola
Minoo na Mamie kwa staili yao
Samawati & CK
Wahida
Zena, akiwa makini kabisa
Mwishoni kabisa baada ya ushuhuda tulitakiwa kutoa sadaka ili kipindi hiki kiendelee.
Bwana na alibariki neno lake

NIMEMPIGA PICHA MKWE

Jana Kinyerezi
Nimempiga picha Mkwe wangu
Bi Samawati Msalya Billy
Maadili na taratibu zinasemaje wadau??
Ni halali?

Monday, July 23, 2012

BONYOKWA HII

Jumamosi.
Bonyokwa nayo inabadilika.
Mwaka 2005 nilipita mitaa hii wakati nikitafuta kura za wananchi.
Jumamosi hii nimepata nafasi ya kupita tena na kujionea mabadiliko makubwa.

HII KALI!!! STIMU HADI MCHANA

Jumamosi mchana, Bonyokwa Kinyerezi
Nikidhania kwangu tu ndio tunawashaga stimu hata mchana.
Kumbe tupo wengi.
Hii niliikuta mchana kweupe Bonyokwa, kwetu Kinyerezi

TEE TETE WITH DADAS

Te a tete na wadada
Jumamosi
Safari Pub, Kinyerezi

Sunday, July 22, 2012

NIDA NA VITAMBULISHO VYA KITAIFA

Bw. Malima, mmojawapo wa waandikishaji
Bibi huyu, she braved the que and sun to join the exercise
Baba Yeyo walikuwepo pia
Kupata kitambulisho siyo mchezo, inabidi uvumilie foleni
Jumamosi
Nilihudhuria zoezi la uandikishaji wa Vitambulisho vya kitaifa pamoja na Minoo.
Mambo ya msingi unapaswa kujua:
Majina yako kamili
Jina kamili la Baba
Jina kamili la Mama
Tarehe yako ya kuzaliwa
Pahala ulipozaliwa
Tarehe ya kuzaliwa Baba
Pahala pa kuzaliwa Baba
Tarehe ya kuzaliwa Mama
Pahala pa kuzaliwa Mama
na mambo machache kadha wa kadha
Mimi nimeshafuzu kujiandikisha




Saturday, July 21, 2012

RAMADHAN KAREEM

Ramadhan moja leo
Mfungo mwema kwa watakaofunga.
Wengine tunasubiria sikukuu ya Idd

PESA SABUNI YA ROHO

Pesa hakika kizungumkuti,
waweza kuandika makala nyingi na ndefu kuhusu pesa
Pesa imekuwepo tokea enzi za Masihi.

Wednesday, July 18, 2012

UWEKEZAJI

Uwekezaji huu
Kawawa Road, Dar Es Salaam
Ni nyumba zilizopata kuwa za wapangaji za NHC

PALE MUDA UNAPOKUWA HABA

 Our Chief Engineer, jana jioni
Eng S K MUSHI
Pale muda unapokuwa haba, na unataka kuwahi.
Boda boda ndio chaguo.
Lakini usisahau kuchukua tahadhari ya USALAMA KWANZA

AFANDE ON DUTY

 AfriCentre jana jioni
Afande lindoni, akipiga macho huku na kule.
Lakini hakuweza kugundua Lens ya Blogger ishamwelekea.

NDEGE WETU DELMONTE

Ndege wetu, kama ilivyo DELMONTE nae ni mjenzi.
Hujenga kila siku na hakati tamaa,
Kesho yake mlango ukifunguliwa nyumba inabomolewa yote.
Lakini maisha yake yameendelea hivo hivo, kujenga kila siku bila kukata tamaa.

Tuesday, July 17, 2012

BONGO DARISALAMA

City view as seen from Itumbi Hotel, Magomeni Mwembechai
Bongo DariSalama yetu inakua na kubadilika kila siku,
Asikudanganye mtu kuwa Nilikuwa kwa Mjomba Darisalama mwaka juzi, Hivyo Jiji hilo halinisumbui.
La hasha ...........................
Hata wa Kinyerezi usipoenda Mjini kati kwa miezi mitatu hivi,
Ukienda utashangaa, na kama siyo tu aibu................ Utauliza hapa ni wapi?