Total Pageviews

Thursday, August 25, 2016

BE AWARE, U - TURN IN STYLE

Hakika Dar Es Salaam yetu inabadilika,
Kwa wageni, hampaswi kuendesha kwa mazoea bali kuzingatia maelekezo.
Unapokuwa unaendesha sambamba na barabara za mwendokasi, unapohitaji kugeuka kurudi ulikotoka (U-Turn), unapaswa kukaa  kushoto na wala siyo kulia kama ilivyo mazoea.
Endesha salama, dereva makini.

Monday, August 15, 2016

GREETINGS FROM MTWARA

Hao ni bwana na bibi Bright Msalya wakifurahia raha ya sabato nyumbani kwao Ligula A Mtwara mara baada ya kutoka kanisani kwenye ibada ya sabato ya yarehe 13/8/2016.

Friday, August 12, 2016

HOME IS THE BEST

Nyamagoti na wadau,
Nakatuba , Ijumaa

LIJUE ZIWA NGOZI

Ziwa Ngozi liko takribani kilometa 38 kutoka Mbeya mjini, kwenye safu za milima ya Uporoto. Ni Mita 2620 toka usawa wa bahari. Ukubwa wake ni Kilometa za mraba zipatazo 3.75
Kuna simulizi nyingi za kale kuhusu ziwa Ngozi, lakini wanasayansi wanasisitiza kuwa ni matokeo ya Volkano.
Ziwa Ngozi halina mto unaoingiza wala kutoa maji. Kuna samaki katika ziwa hili japokuwa hakuna shughuli za uvuvi kutokana na ugumu wa kulifikia na pia nyenzo za uvuvi.
Ni mojawapo ya vivutio vya utalii nchini mwetu.

Tuesday, August 2, 2016

KWETU KITUNDI

Usafiri wetu Kitundi - Nachingwea.
Picha toka kwa Mdau Silla aliyetembelea Nachingwea karibuni.

WADAU WATEMBELEA ENEO LA TUKIO LA AJALI

Wadau wa blog yetu leo walipata fursa ya kutembelea Shule ya msingi Migungani. Pahala hapa kwenye mti huu ndipo alipopatia ajali ya kudondoka kutoka juu, Bw. Maingu Baruku majira ya saa Tisa alasiri, Alhamisi tarehe 28 Julai 2016.
Akiwa huko juu kileleni akichuma maua kwa ajili ya kufyonza juisi iliyomo, tawi alilokuwa amelikalia lilikatika na mwenyewe kuanguka hadi chini.
Inakisiwa ni wastani wa kina cha Mita saba.