Ama kwa hakika mwanamme unapaswa kusifiwa kwa kuchapa kazi, ili kuitunza vema familia na wategemezi wengine.
Pichani, Mwanamme akiwa kazini jana mitaa ya Msimbazi, Kawawa Road.
Kwa uchache mzigo unakadiriwa siyo chini ya Kgs 500 (Nusu Tani)
Ndege wetu, kama ilivyo DELMONTE nae ni mjenzi.
Hujenga kila siku na hakati tamaa,
Kesho yake mlango ukifunguliwa nyumba inabomolewa yote.
Lakini maisha yake yameendelea hivo hivo, kujenga kila siku bila kukata tamaa.
City view as seen from Itumbi Hotel, Magomeni Mwembechai
Bongo DariSalama yetu inakua na kubadilika kila siku,
Asikudanganye mtu kuwa Nilikuwa kwa Mjomba Darisalama mwaka juzi, Hivyo Jiji hilo halinisumbui.
La hasha ...........................
Hata wa Kinyerezi usipoenda Mjini kati kwa miezi mitatu hivi,
Ukienda utashangaa, na kama siyo tu aibu................ Utauliza hapa ni wapi?