Wednesday, September 28, 2011

TASWIRA TOKA BEACH YA BAGAMOYO

Dhow packing
Once Sultanate residence

Its a beach near current customs house

Sea view

In memory of hanging tree, at BADECO beach hotel

I once worked here in 1991, as secondment from District council before the Hotel was privatised

Tuesday, September 27, 2011

NASHINDWA KUFIKIRIA ITAKAVYOKUWA

Nikiwa nimepanda nyuma ya Pick up mitaa hii ya Uhuru/Kawawa na Olympus yangu mkononi nilivutiwa na taswira hizi za msongamano wa magari na watu.
Najiuliza,
Kila siku Bongo Dar Es Salaam watu wanaongezeka.
Miundo mbinu ni ile ile
Resources ni zile zile
Maeneo ndiyo yanazidi kufungwa.
Ni nini kitatokea miaka 15 - 25 ijayo?
Nashindwa kabisa kufikiria itakavyokuwa.
Ndiyo maana natamani sana kuweko Nakatuba kuanzia 2020


An EVENING AT KITUNDA

Maandalizi ya safari ya Nakatuba yanaendelea,
Jumapili nikapata nafasi ya kuwapitia wadau wa Kitunda kupata mipangilio.
Wadau wana shauku kubwa ya kujiunga kwenye safari hii.
Ni Malembo au Beria, mimi sitaki kuingilia ugomvi wao. Lakini likely mmoja wao tutakuwa nae.

Kutembelea ndugu kuna raha yake,

Hapa Ankal ilikuwa furaha tupu ambayo hakuweza kuificha............
Msosi wa Vitamini ulikuweko
Ankal mwingine salamu yake hupatikana kwa mbinde
Lakini wakati wa kuaga kuondoka, hujongea...
Posho toka kwa Uncle

Lunch point

We are frequently using this place as our lunching point


The Lincon Car outside had been as an icon of the place.



It serves also as Drinking place
and Functions halls

Friday, September 23, 2011

SIKU YA MDAU EDDY 20.09 NA KIZUNGUMKUTI CHAKE

Mdau Tabi, aliyetukumbusha siku hii
Belly Jnr, Belly Snr ndiye atatukatia kitendawili hiki
Mdau na Mzee CK, mzee mwenye data
Juzi nikapata mail fupi toka kwa Ankal,kama hapa chini:
"Dear Uncle,
natumaini Mungu amewajalia afya na baraka. mie sijambo, namalizia mitihani sasa.
nilijaribu ku-post birthday ya Eddy kwenye blog, lakini nimejikuta sijui jinsi ya kufanya. hivyo basi nikaona ni vyema nikushtue ili uiweke. ilikuwa jana 20/august.
bye for now,
Tabitha"

Mbio mbio nikitahayari kumsahau Uncle nikaenda ku confirm na Pamphlet ya Great Couple.
na huko nikakuta haya

ORODHA YA WAJUKUU
1. Msalya George 06.06.1973 Belly
2. Mnyaga Eddyson 23.08.1976 Belly
3. Msalya J 13.05.1983 Billy
4. Bhituro Lulu 21.06.1985 Bright
5. Manyori 17.11.1985 Billy
Nikawa nimekwama.............
Nikamtafuta CK, ...............simu uliyopiga haipatikani.......
Nikamtafuta Mwl Belly................simu uliyopiga haipatikani..........
Nikamtafuta mtoto mwenyewe......................simu uliyopiga haipatikani...........

Lakini jana hatimae nikampata mtoto.
Baada ya kumdodosa akaniambia....
"Ni kweli, 20/09 ni siku yangu. Nilijisahau tu mpaka nikashituliwa na Mama BJ"
Lakini je ni August au ni September?
Bado kuna maswali yanahitaji majibu.
Kwa kuwa siku hiyo MDAU HAKUWEPO, bado nitaendelea kudodosa dodosa kwa Mzee CK na Mwl Belly Snr.
Au mdau yeyote aliye na info za uhakika.
Pamoja na hayo,
kwa wakati huu tuendelee na

HAPPY BIRTHDAY
DEAR EDDY

Monday, September 12, 2011

TUTABANANA HUMU HUMU

Dar Es Salaam yetu ni njema, atakae na aje.
Kuishi Dar kunataka juhudi za binafsi.
lakini nafasi iko kwa kila mmoja mwenye nia ya kufanya kazi kwa juhudi.
Ukitembeza maji............pesa
Ukiuza Ubuyu.................pesa
Ukikata nyasi..................pesa
Kuzibua vyoo...................pesa
Uokote chupa..................pesa
Uokote Nylon..................pesa
Uuze utumbo wa kuku........pesa

Friday, September 9, 2011

SIMULIZI ZA KALE ZA BABU GIZA

Zamani zile, watoto wakisimuliwa wapatavyo usingizi............

Babu Giza hupita akizungukazunguka na ndoo yake ya rangi

Akigundua hujamuona, huchukua brashi yake na kukupaka rangi machoni.

Kwishnei....

Utasinzia, ndio usingizi namna hiyo.

Siku hizi ofisini kwetu wanaendeleza simulizi hizi kwa namna yake.

NGELEJA kapita........................

Akipita hujamuona anachukua UMEME wake.

inabakia huna kazi ya kufanya, plus joto la Dar

Lazima kausingizi kakunyemelee tu........... Imebakia najiuliza na huko mjengoni nako...............

Ulinzi upo wa kutosha kumuzuia Babu Giza kuingia bila kibali

Hali ya hewa mulua kabisa, full kiyoyozi

Ni simulizi gani inatumika?

Waheshimiwa wanafuatilia kwa makini,

Waheshimiwa wanatafakari kabla ya kuamua kuunga mkono au kukataa hoja.........

Lakini yote ni yote tu.........
iwe Babu Giza

au Ngeleja..

kausingizi hako katamu huwa hakaepukiki





Wednesday, September 7, 2011

VIKAO VYA MAANDALIZI - SHABANI LABAN MAGWE

Vikao vya maandalizi ya Harusi ya Bw. Shabani Laban Magwe vinaendelea kule Kizota bar, Sabasaba. Na majuzi tu ilikuwa kikao cha nne.


Tarehe ya Harusi sasa iko tayari, ni 26 Novemba 2011
Na Sherehe itakuwa kule ukumbi wa Baraza la Maaskofu Kurasini

Saturday, September 3, 2011

KAZI NI KAZI

Nimevutiwa sana na picha ya Mjasiriamali huyu anavyochapa kazi. Picha imetoka blog nyingine.
Imenikumbusha Nakatuba.
Laiti ningeiona kabla ya kuanza usombaji wa matofari ya Mzee CK.
Hakika ingerahisisha sana.

Friday, September 2, 2011

KATIBA YA CHENDANE FOUNDATION IKO TAYARI

CHENDANE FOUNDATION LOGO
Siku ilianza kwa shughuli za kawaida za kila siku, kama hii ya kwenda kutafuta maji

Baadae wajumbe waliwasili, na kikao kikaendelea kwa mahudhurio ya kuridhisha ya wajumbe.

Wakapitia kifungu kwa kifungu mwanzo hadi mwisho.

Penye wengi, haliharibiki jambo

Baada ya mapitio, marekebisho na majumuisho...................

Imekubaliwa Katiba inaanza kazi rasmi tarehe 01 OKTOBA 2011

Kulikuwa na haki kabisa ya kufurahia Katiba tuliyokuwa tukiitafuta kwa muda mrefu sasa.

Kama kawaida kikao kilikuwa na wajumbe wapya,


MGENI TOKA BUNDA Mr SUPER

Idd Pili, nikawa na bahati ya kupata mgeni mwingine toka Bunda,
Si mwingine ni Engineer Super Mathias Chisute Mteki.
Sasa mjasiriamali na mfanyabiashara katika bidhaa za umeme kule Bunda
Akapata nafasi ya ku " pay respect" kwenye Kaburi la Kamanda Josia Mwayai Msalya


Mgeni njoo, mwenyeji apone.................

Kutoka huko, mtoto wa Mama akanikumbuka kwamba nililia sana peke yangu wakati huo

akapata nafasi ya kunipoza angalau moja moto........ na moja baridi....