Friday, September 23, 2011

SIKU YA MDAU EDDY 20.09 NA KIZUNGUMKUTI CHAKE

Mdau Tabi, aliyetukumbusha siku hii
Belly Jnr, Belly Snr ndiye atatukatia kitendawili hiki
Mdau na Mzee CK, mzee mwenye data
Juzi nikapata mail fupi toka kwa Ankal,kama hapa chini:
"Dear Uncle,
natumaini Mungu amewajalia afya na baraka. mie sijambo, namalizia mitihani sasa.
nilijaribu ku-post birthday ya Eddy kwenye blog, lakini nimejikuta sijui jinsi ya kufanya. hivyo basi nikaona ni vyema nikushtue ili uiweke. ilikuwa jana 20/august.
bye for now,
Tabitha"

Mbio mbio nikitahayari kumsahau Uncle nikaenda ku confirm na Pamphlet ya Great Couple.
na huko nikakuta haya

ORODHA YA WAJUKUU
1. Msalya George 06.06.1973 Belly
2. Mnyaga Eddyson 23.08.1976 Belly
3. Msalya J 13.05.1983 Billy
4. Bhituro Lulu 21.06.1985 Bright
5. Manyori 17.11.1985 Billy
Nikawa nimekwama.............
Nikamtafuta CK, ...............simu uliyopiga haipatikani.......
Nikamtafuta Mwl Belly................simu uliyopiga haipatikani..........
Nikamtafuta mtoto mwenyewe......................simu uliyopiga haipatikani...........

Lakini jana hatimae nikampata mtoto.
Baada ya kumdodosa akaniambia....
"Ni kweli, 20/09 ni siku yangu. Nilijisahau tu mpaka nikashituliwa na Mama BJ"
Lakini je ni August au ni September?
Bado kuna maswali yanahitaji majibu.
Kwa kuwa siku hiyo MDAU HAKUWEPO, bado nitaendelea kudodosa dodosa kwa Mzee CK na Mwl Belly Snr.
Au mdau yeyote aliye na info za uhakika.
Pamoja na hayo,
kwa wakati huu tuendelee na

HAPPY BIRTHDAY
DEAR EDDY

1 comment:

  1. Uncle, tarehe ni 20 Sept. Nimejikuta mwezi huu wote nauita 'august' naona hata kwenye msg yangu bado nimefanya hivyo.
    Matafute Mwl Belly atakupa full story.

    ha ha ha ha ha

    ReplyDelete