Friday, September 9, 2011

SIMULIZI ZA KALE ZA BABU GIZA

Zamani zile, watoto wakisimuliwa wapatavyo usingizi............

Babu Giza hupita akizungukazunguka na ndoo yake ya rangi

Akigundua hujamuona, huchukua brashi yake na kukupaka rangi machoni.

Kwishnei....

Utasinzia, ndio usingizi namna hiyo.

Siku hizi ofisini kwetu wanaendeleza simulizi hizi kwa namna yake.

NGELEJA kapita........................

Akipita hujamuona anachukua UMEME wake.

inabakia huna kazi ya kufanya, plus joto la Dar

Lazima kausingizi kakunyemelee tu........... Imebakia najiuliza na huko mjengoni nako...............

Ulinzi upo wa kutosha kumuzuia Babu Giza kuingia bila kibali

Hali ya hewa mulua kabisa, full kiyoyozi

Ni simulizi gani inatumika?

Waheshimiwa wanafuatilia kwa makini,

Waheshimiwa wanatafakari kabla ya kuamua kuunga mkono au kukataa hoja.........

Lakini yote ni yote tu.........
iwe Babu Giza

au Ngeleja..

kausingizi hako katamu huwa hakaepukiki





No comments:

Post a Comment