Wednesday, April 6, 2011

ANOTHER KIWANGWA TRIP

Jumamosi iliyopita nikalazimika tena kwenda kutembelea Kiwangwa, Bago Talawanda Road project
safari hii nilipaswa kwenda fasta fasta, maana niliondoka ofisini saa nane, na nilipaswa kwenda na kugeuka siku hiyo hiyo kuwahi ratiba nyingine ya Jumapili
Bagamoyo mji wenye mambo mengi, sikukosa japo kumbukumbu ndogo. Hivo baada ya kupata lanchi yangu pale Top Life, nikapitia Caravan Serai kupata walau kumbukumbu hii.
Hapa ndipo watumwa kutoka Bara wakifikia kabla ya kuanza safari ya majuu.
hapa ndipo neno Bwaga - Moyo, "Bagamoyo" leo lilipotokea.
Nikapakumbuka maskani yangu pia miaka ya 1985 - 1989.
Nyumba ya Mzee Mambo, enzi zile wapangaji kama kumi hivi au zaidi. wenye idadi ya watu zaidi ya 50.
Nakumbuka foleni ya kuoga chooni asubuhi, na halaufu ya Mnazi kama Mangi atakuwa ameshaingia humo. Hapa nawakumbuka Mzee Mhando, Mzee Peter, Kaburi na Emmy
Ningekuweko hadi leo ningekuwa sasa ni jirani na Mkulu wa Nchi. nyumba ya tatu tu hapo mbele kwenye bendera ya kaya.
Hakika sasa panahitaji ukarabati wa nguvu
Tunaingia Makurunge, crossing River Ruvu
Mtu Ruvu
Na njiani picha za kumbukumbu na maasai wa Kidomole
Hatimae Maskani ya wadau Kiwangwa
Mwanzo wa mradi
Hapa hakuna njia, daraja imeenda na maji kwa hiyo lazima kuishia hapa na kuwasubiri wadau watakapomaliza kazi huko waliko.

No comments:

Post a Comment