Total Pageviews

Monday, January 8, 2018

MJI KASORO BAHARI

Nimetembelea tena Morogoro baada ya muda mrefu kupita,
Morogoro imebadilika sana,
Hakuna maji ya kutiririka vilimani tena,
Uoto umeondoka milimani,
Hakuna Mziki tena,
Lakini Morogoro inakua,
Majengo Makubwa na Mazuri yanamea,
Mji Unatanuka.
Na Stendi nzuri na ya kuvutia, Stendi ya Msamvu.

FINAL TOUCH

Masaa machache kabla ya Kuelekea Shuleni Kitungwa,
Usafi wa Kucha unazingatiwa.

Kihonda, Morogoro
Jumapili

KWAHERI YA KUONANA

Wapendwa Minoo na Penina,

Leo ni siku muhimu kwenu, baada ya kumaliza masomo ya msingi sasa mnaelekea Kitungwa kuendelea na maisha ya shule ya aina nyingine, masomo ya sekondari.
Tunasononeka kuwa sasa hatutakuwa nanyi  nyumbani kila siku kila saa, hatuwezi kucheka na kufurahi pamoja tena, mtakuwa mbali nasi. lakini twafarijika kwamba mnapata fursa nyingine muhimu kwenu katika kuyafikia maarifa.
Kwa kuwa Shule pekee, twaamini mtajifunza mengi ikiwemo kujitegemea na kufanya maamuzi kwa ajili ya maisha yenu ya usoni.
Sisi familia tunawatakia kila la kheri na fanaka kwa hiyo miaka minne mutakayokuwa Kitungwa.
KWAHERI YA KUONANA.

Msalya - MyFamily
Jumapili 07 Jan 2018

Wednesday, January 3, 2018

Monday, January 1, 2018

WHEN NEW YEAR GOES BAD


Pale umepenya mkesha wa Mwaka Mpya,
Unajipanga kwa ratiba ya New Year,
Then something goes wrong!
Kinyerezi kwa Chaibora,
Mchana wa Mwaka Mpya.

Thursday, December 28, 2017

TEMBEA UJIONEE

Mwanamuziki Nguli nchini, Hayati Remmy Ongala alipata kuimba "Tembea ujionee"
Unaweza kuwa umepata kutembelea Baa za aina mbalimbali, Miti ikiwa imepandwa karibu kuzizunguka au hata ndani yake kwa ajili ya kupendezesha mazingira.
Lakini sivyo kwa "The Big BaoBab Tree Bar" mambo ni tofauti hapa. Baa hii iko ndani ya Mti mkubwa wa Mbuyu, wenye maelfu ya miaka na unaosadikika kuwa Mti Mkubwa kuliko yote Duniani.
Hapa ni katika mji wa Modjadjiskloof, katika Jimbo la Limpopo nchini Afrika Kusini.
Hakika Tembea ujionee........

Source
Mitandaoni

50 th WEDDING ANNIVERSARY


Miaka Hamsini iliyopita,
Naam, Nakubali kukupokea katika Shida na Raha.
Nusu Karne sasa, Uhusiano unazidi kukua na kuwa bora zaidi.
Kila la kheri Bw na Bi Lucas Daniel Gunze.

Recently in Bariadi.