Total Pageviews

Wednesday, November 29, 2017

TAFAKARI KABLA YA KUTENDA

Tafakuri ya Mbuzi kabla ya kuvuka Daraja,
Kigogo Mkwajuni,
Leo Asubuhi

Tuesday, November 28, 2017

KISA CHA KALENDA

Hapo zamani,
Mwaka 1752, Waingereza walipokwenda kulala tarehe 2 Septemba lakini walipoamuka kesho yake ilikuwa tarehe 14 Septemba.
Kulikoni,
Siku 11 zilikuwa zimeondolewa kwenye Mwezi wa Tisa ili kuendana na Sheria mpya ya Kalenda.
"Calendar (New Style) Act of 1750"
Huu ni Mwezi Waingereza walihama kutoka matumizi ya Kalenda ya Julian kwenda Kalenda ya Gregorian.
Pia katika Kalenda ya Julian, mwaka mpya ukianza Tarehe 1 April. Sasa hata baada ya mabadiliko Waingereza wengi wakiendelea kusheherekea Mwaka Mpya April mosi. Kwa kuchukizwa na hilo Mfalme akawa ametoa amri kuwa wote wanaoendelea kusheherekea Mwaka Mpya April Mosi kuitwa Wajinga, Na kuanzia hapo April Mosi imejulikana kama Sikukuu ya Wajinga.

"Kutoka Mitandaoni"

Saturday, November 25, 2017

MAMA MKUBWA BIRTHDAY CELEBRATIONS

Photos from Mtwara Kwetu,
Hii na namna ilivyokuwa 16 Novemba 2017,
Wakati Bi Jennifer Simbua Bright akiadhimisha miaka kadhaa ya kuzaliwa kwake.

Friday, November 24, 2017

KINYEREZI KWETU

New Kinyerezi Bus Stand,
Panorama Photo shoot by Blogger

FOCONA RAFIKI WA MAZINGIRA MTWARA

Forum for Conservation of Nature, Mtwara HQ wanazidi kuchanja mbuga katika uhifadhi wa mazingira.
Pamoja na kuwa na Vitalu vya miti ambayo huisambaza baadae kwa jamii, Mitaani wameeneza ujumbe wa kuhimiza utunzaji wa Mazingira kama vile kutokutupa takataka ovyo na upandaji wa miti.

Thursday, November 16, 2017

Tuesday, November 14, 2017

UOGAJI KATIKA SAUNA

Wajua Sauna ni nini?
Sauna, kama Bafu la kuogea ni ustaarabu wa miaka mingi wa Watu wa Finland. Karibu kila nyumba nchini Finland in Sauna yake.
Hiki ni chumba maalumu ambacho hupashwa joto kwa Kuni, Mkaa, Umeme au Gesi kwa ajili ya kuweka Mvuke, Moshi au Joto kwenye Sauna.
Watu huingia humu kuoga mvuke, Mvuke huu husababisha mwogaji kutoa jasho. Na kwa kutoa jasho huamini mwili husafishika na kuimarika.
Sauna yaweza kutumiwa na mtu mmoja mmoja au watu wengi kwa pamoja, wa familia moja au ofisini
Kila nyumba, na kila Ofisi ina chumba cha Sauna
 Chumba cha Sauna, Turku University Science Park.