Total Pageviews

Wednesday, October 17, 2012

LEO NI SIKU YA MDAU NEEMA

 
Leo 17.10.2012
Ni Siku ya mdau NEEMA BRIGHT K MSALYA
Mdau anatimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa leo hii
HAPPY BIRTHDAY 
Dear NEEMA

Kuna mnuso baadae hii leo jioni kuendana na siku hii maalum ya mdau huko Kipunguni.
Blogger wenu nimekwisha fikishiwa mualiko, kwa wale ambao hamtaweza kuhudhuria, basi Inshallah NITAWAWAKILISHA
                                                                                                                                                                               

Monday, October 15, 2012

MTANUAJI ANAPOPIGWA BAO

Utii wa Sheria bila shuruti,
Lakini haikuwa hivo kwa Dereva huyu wa Daladala aliyeamua kutanua.
Nyerere Road, Scania Vingunguti last friday

MADE IN UBUNGO

Truck made in Ubungo Maziwa, Dar Es Salaam,
Jumamosi

Friday, October 12, 2012

FOLENI KAMA KAWAIDA

 
 
 
 
 
Ni kawaida sasa barabara zetu mida hii ya kuanzia alasiri.
Hata jamaa zangu wa TZR leo wamekumbana na adha hii, maana hata service road zote zilikuwa zimefunga
Kawawa Rd, Msimbazi Mission masaa machache yaliyopita

Thursday, October 11, 2012

BON VOYAGE MWAYAI

 
 
 
 
 
 
Mzee Mwayai yuko safarini akirejea Bunda baada ya ziara ya kusafisha macho jijini kwa takribani wiki mbili.
Ameondoka alfajiri hii na Musoma Express, na Mungu akijalia safari ikaenda salama, basi mida ya saa nne usiku atakuwa mjini Bunda.
Wadau wa Bongo jana walipata wasaa mfupi wa kuwa nae kumuaga na kupata mawili matatu.
Hakika ni faraja sana unapopata nafasi ya kuwa na Wazee hawa ukapata mawili matatu ya busara na hekima kutoka kwao.
BON VOYAGE Mzee MWAYAI

Wednesday, October 10, 2012

NYOMI

Ndivyo ilivyo Bongo yetu,
mvua kidogo, hakuna gari za abiria barabarani, vituo vinafurika
Leo asubuhi, Kawawa Road, Machinga Complex

Monday, October 8, 2012