Total Pageviews

Tuesday, January 18, 2011

SAFARI YETU KARUKEKERE KWA NYAMWEYA - PART ONE

Wadau wawakilishi wa Wadau wa Dar waliamua vekesheni iende kwa kuunga unga,
Mdau Chief Photographer wa Blog aliongoza msafara................. kazi nzito lazima kutafakari
Mdau akiwazia, huko niendako..........................
Kukoje??????

Na wengine waliivutia pumzi vekesheni yenyewe
"Defostration" kila sehemu............
Naikumbuka na kuililia Nakatuba kwa jinsi ilivyochakachuliwa siku hizi.
Bila ya shaka ilianza hivi hivi
Wadau waliweka dhamana yao kwa mkongwe wa njia ya Dodoma - Shabiby Line
Breki ya kwanza ikawa Dom
Wadau wakajichanganya
Kulipokucha safari kama kawaida ikaendelea
Bunda Bus, mtoto wa nyumbani zamu hii akapewa dhamana
Bibi Penina alikuwepo kuwapokea walipofika PIDA
Furaha ilioje kukutana na wadau wengine huko
Na kushiriki pamoja katika Sabato ya Bwana

Friday, January 7, 2011

NAKATUBA IN 1930s

Hii stori imebidi niitoe kwa jinsi ilivyotumwa kwangu na Mwanasheria.
Hizi ni Dondoo zilizopatikana wakati wa Vekesheni ile ya kupanda Beacon za Msalya kule Nakatuba.
Nimefanya edit chache sana pale ilipokuwa ni lazima tu.


UKOO WA CHISAKA MSALYA MASEME CHIMORI MANYORI

Ikumbukwe kwamba MSALYA ni jina la “lumula” yaani ali maarufu.

Lilitokana na kuvuruga mipango ya wengine katika mashindano ya ngoma na hatimae kuwashinda. Katika hili msaidizi wake mkuu alikuwa Bwana Manyori.

Siku ya kikao “mwose” alioutumia katika mashindano ya ngoma za kitamaduni ulionyeshwa, uke pale nyumbani kwa Bwana C. K. Msalya.

Angalizo: Kule Kenya jina hili huandikwa Musalia au Musalya. Awali mzee CK akitumia Musalya naona baadae akaamua kubadilisha.

Chimori alimzaa Maseme, Maseme akamzaa Msalya na Nyalimbi.

Chisaka akamzaa Nyabhwangu.

WATOTO, WAKE NA WAJUKUU WA MSALYA

MTOTO - MAMA

1. Bhajalaki - Mwango

2. Manyori - Mwango

3. Kulwijira C K - Bhituro

4. Mwayai - Bhituro

5. Nyanjura - Buhinda

6. Gabhaseki - Nyamata

7. Chausiku - Kamwanyi

8. Taabu - Kamwanyi

9 - Mwananonga kutoka Tabora

WATOTO NA WAJUKUU

  1. Bhajalaki akamzaa Mkwaya kwa bwana....
  2. Nyanjura akamzaa Goodluck na Tereza kwa bwana.... Goodluck amezaa Christopher na Nyanjura kwa mama.....
  3. Manyori hakuzaa
  4. Gabhaseki kwa bwana Mafuru akazaa: Tatu, Gasige, Bhulesi, Siri, Daniel, Adamu, Grace, Msalya, Taabu na Salya. Kwa bwana William akazaa Mafwolo.
  5. Kulwijira CK kwa mama Penina Nyabhutwema akazaa: Belly, Bright, Billy, Better (marehemu), Beria, Baruku, Bithia, Sarah (Bora), Bahati (Nyang’oko), Bilshani na Makubhi (Baasha)
  6. Mwayai akazaa kwa mama Nyakamoga(Nyanyingu): Jumanne, Josiah, Jackson, Nyamumwi (marehemu), Kabhajilo, Kamoga, Munyaga (marehemu), Maseme na John. Akazaa kwa mama Mwajuma Kagele na pia akazaa kwa mama Nyamasisi: Jeradi, Silas na Msalya (Tall)
  7. Chausiku akazaa kwa bwana Yakobo Victoria , Monica, Zainabu (marehemu), Nyangeta, Bharongo na kwa bwana Zakaria akazaa Sikujua, Mariam na Msalya.
  8. Taabu akazaa kwa bwana Mapigano : Mariam, Kasala, Msalya na Nyabhutache.

WALIOPUMZIKA KWA BWANA C. K. MSALYA

1.Chisaka Msalya Maseme 1895 - 4/6/1966

2.Better Nyamalelo Kulwijira Msalya 27/12/1961 – 17/1/1985

3.Baraka Bilshani Msalya 1/3/2006 – 4/12/2007

4.Mujigu Nyamisango Bhaseki 1920? – 29/1/2009

5. Munyaga Mwayai Msalya Septemba 1982 – Julai 1983

WALIOPUMZIKA KWINGINEKO

  1. Bhituro, Bhusambala kwa Chihalata
  2. Sarah Musema, Kitegule AIC Cemetery
  3. Bhajalaki Msalya, Ukerewe
  4. Manyori?
  5. etc

WAZEE WALIOFIKA NAKATUBA, NAMALEBE NA KITENGULE MIAKA YA 1936 HADI 1937 PAMOJA NA MZEE MSALYA MASEME:

  1. Chisaka Msalya Maseme 1937
  2. Matekere Jorwa June 1936
  3. Gwang’okolo Gwalebha
  4. Malekela Nyachemo 1937
  5. Makene Matoyo
  6. Kasuu Mughobha
  7. Chamata Mulengela
  8. Semba
  9. Mtaka
  10. Kongola Nyamusola
  11. Magesa Kasesela
  12. Maguge
  13. Mutandu
  14. Magesa Kubhilima
  15. Kubhoja
  16. Munyaga Lukonge
  17. Muselele
  18. Mahambo
  19. Matiku
  20. Muyengi
  21. Bwire Makongo
  22. Mukama Bhusumbilo
  23. Musumari
  24. Bhuswike

SIKU YA MDAU 08.01.2011

Hakika siku, wiki, miezi na hatimae miongo mingi imepita..............................
Kesho ni siku ya Mdau
Karibuni wote kushereheka kule kwetu Kinyerezi
08 January 2011

Tuesday, January 4, 2011

MAMBO YA USAFIRI WA DAR

Foleni kwenye usafiri wa Dar zimekuwa ni kero, kero.......................
Wadau kwa kuliona hilo, na changamoto ya Bodaboda ya Chief Photographer,
nao kwa taratibu wanajiandaa kubadilisha aina ya usafiri.
Lakini kwa usalama kwanza, wakaona ni bora kununua kabisa Helmet kabla ya kupata Bodaboda.
Hapa Helmet ikijaribiwa kama inafaa...............
Nami nawatakia kila la kheri kwenye maandalizi yao

OFFICIAL VISIT TO KIWANGWA

Juzi Mwaka mpya baada ya kutoka kanisani nikawa na Trip ya kwenda Kiwangwa - Bagamoyo.
Kijiji maarufu sana kwa ulimaji wa Mananasi.
Kampuni yetu imefanikiwa kupata kazi huko ya ujenzi wa Barabara za vijijini yenye urefu wa km 20 hivi.
Kinokia kikawekwa standby



Madhari poa

MDAU AMINA-TEREZA (Minoo) GOES TO SCHOOL

Leo ni siku muhimu kwa mdau Minoo, mziwanda wa kule kwetu Kinyerezi .

Ni siku ya kuanza safari ndefu ya maisha ya shule.

Na leo aliamuka mapema sana kwa hamasa

Maandalizi bila kuzembea

akipigwa tafu hapa na pale





Final touches
and there the Journey starts

Kila la kheri Minoo katika safari hii ndefu, ingawa kwa sasa sidhani kama unaitambua vilivyo

..................MOLA NA AKUANGAZIE..................

Sunday, January 2, 2011

SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA KAGOSHIMA

SALAMU ZA MWAKA MPYA 2011 ZA WADAU KUTOKA KAGOSHIMA KWENDA KWA WADAU WOTE WA BLOG HII