Sunday, August 13, 2017

SHULE YETU NAMALEBE: KUKUMBUKA TULIKOTOKA

Namalebe Primary School on Google Maps: -2.109605,33.435483
Darasa la Awali kabisa 1949 lilijengwa hapa
Karibuni  nimepenyezwa wazo na Wadau wa Elimu, Ni wadau  wa Elimu waliowahi  kusoma shule ya msingi  Namalebe  iliyopo kata ya Kibara , Jimbo la Mwibara.  Shule  ya Msingi  Namalebe  ilianzishwa yapata miongo saba iliyopita, Ilianza mwaka 1949 ,hivyo panapo majaliwa itakapofika 2019 shule hii itakuwa inatimiza miaka 70 ya kutoa Elimu.
Wadau wa Elimu   wanaona ni wakati wa Wasomi wote waliopitia hapo kurudisha kidogo kama ishara ya shukrani .Wadau wanafikiria ni vyema kuwa na Sherehe za Platinum Jubilee kutafakali ilikotaka  Namalebe, ilipo na inapoelekea. Namalebe ndiyo shule ya mwanzo kabisa katika jimbo la Mwibara, lakini pamoja na kukaribia miaka miongo saba, bado iko nyuma sana kulinganisha na shule zilizokuja baadae.
Binafsi kama mdau, tena mwenye rekodi ya kuwa kati ya wadau waliosoma kwa miaka mingi Namalebe nawiwa,
Na hata  nilipotakiwa na Wadau wa Elimu wa Namalebe kuweka makala mtandaoni ya uchokozi wa kutafutana wote waliopitia shule ya msingi Namalebe, sikusita…………..
Lakini baadae nimejikuta njia panda,sijui pa kuanzia. Tutafurahi sana kupata habari zako mdau wa Elimu wa Namalebe. Tafadhali tutumie mawasiliano yako, au namna tunavyoweza kukufikia au mapendekezo yako yoyote. Nyumbani Namalebe na Nakatuba Bwana Tungura Misana Mkhoi ( Class of 1963 ) Na Goodluck M. Ngalya ( 0629 417631 ) wako tayari kupokea habari uliyonayo kuhusu Namalebe.
Bw  Nyande Misana Mkhoi ( 0713 730 232 ) Kanda ya kaskazini anapokea habari yako mdau kama ilivyvo kwa Mwl Msataafu Belly Msalya ( 0759 390 575 ) aliyeko Bunda. Tuna Mratibu Kanda ya Kusini Bw. Bright ( 0717 404 885 )  na Dar Es Salaam tunao Bw Machele ( 0754 824375 ) na mimi mchokozi wa makala hii kwenye namba  0713 236 990.

Tupe habari yako, maoni na ushauri kusudi tujipange  vipi kwa ajili ya Platinum Jubilee ya Namalebe mwishoni mwa 2019.
Mr Ernest Munubhi Magoti, Early Schoolers 1949
NAMALEBE 1949
Kiguu na njia kutafuta habari za Namalebe.
Mabhui Merafulu, Majita. Ndipo makazi ya mstaafu na sasa mkulima Bw.  Ernest Mnubhi Magoti. Mzee Magoti anaikumbuka Namalebe 1949 ilipoanza. Anakumbuka jinsi wajenzi wakivuna miti Kurwirwi ( Nyasuruli ) kwa ajili ya ujenzi wa shule. Wakati huo wakikaa kwa Mzee Malekela Nyachemo. Mwanafunzi mwenzie ni Binti wa Malekela, Bi Nyabwire, sasa mjane wa Marehemu Yoel Masano makazi yao Namuhula.
 Marco Riganya House Late 1960
Sylivester and Martin resided here.
 Mwl Eliab Mkama residence
Makaranga Ndimila Residence
WALIMU
Siku zinaenda mbio, Namalebe inasonga. Walimu wengi wamepita hapa. Si rahisi kuwakumbuka wote kwa mara moja.
Sospiter Malegesi alipita hapa, Marco Riganya Mwalimu Mkuu kwa wakati wake, maarufu kwa Scooter yake kijijijni, lakini nadra kukutana na wanafunzi maana wakiisikia kabla mtaani. Siku moja moja akiingia pembezoniya kijiji kwa mawindo ya Kanga na Rifle yake.
Faustine Makaranga Ndimila, Specialist kwa wanafunzi wanaoanza. Kama unakumbuka vizuri hupokelewi mpaka mkono wa upande mmoja umeshika sikio la upande wa pili kwa kupitia kichwani. Mzee huyu ndiyo baba yao na Marehemu Godfrey na Albert na Binti Felista ambae mara ya mwisho tulikutana JKT RUVU, Mwl Makaranga nasikia makazi yake yako Bunda kwa sasa, Mwl Haruni Pamba, Seif Mkome maarufu kwa hesabu ya kichwa. Mwl Chibiriti , mtoto wa mjini. Young and ambition Teachers Sylivester and Martin. Sylivester alikuja baadae kuwa mume wa mwanafunzi Penina Malegesi. Bahati ilikua upande wake, sheria ya miaka 30 ilikua haijaanza.
Mwalimu Mkuu wa enzi zetu Marehemu Eliabu Mkama The Linguistic Teacher na kitabu chake kisichochuja “Common mistakes in English” pamoja na Mkewe Mwl Damali Mkama mbobezi wa Hesabu na Maarifa ya nyumbani. Not the last Mzee wetu Alphaxard Maleka Matekere akirejea  nyumbani Namalebe miaka ya katikati ya 70 bila ya shaka akijiandaa kustaafu baada ya kulitumikia taifa miaka mingi sehemu mbalimbali.
Ujio wa Mzee Maleka ukiwatia kiwewe wanafunzi kuwa ni Mwl mkali. Kumbe hofu tu, hakua tena na mkono wa kuchapa viboko, akawa Mwl mshauri kwa walimu na wanafunzi wote, wanae Marehemu Lawi na  Jamhuri ndio wakapata nafasi ya kuja  kumalizia elimu yao ya msingi Namalebe. Jamhuri a.k.a  Maradona ndie amebakia icon ya Boma la Mzee Maleka kijijini kwetu.
NAMALEBE NA STD V
Baada ya miaka 22, Hatimae Namalebe inapata darasa lake la tano la kwanza. Kwa furaha hiyo  wanafunzi wote waliofanya mtihani wa kumaliza drasa la nne wanachaguliwa kuendelea na darasa la tano. Tukiwakumbuka wadada hawa ni pamoja na Akisa Samwel Ngalya, Sherida Mgeta, Penina Manyama, Chausiku Nyamwaga, Dorika Muyemba na Penina Maregesi aliye kuja baadae kuwa mke wa Mwl Sylivester. Kwa mara ya kwanza pia Namalebe ikapata wanafunzi kutoka Mkoko na Igundu. Wanafunzi Nicodemus na Mtaka kwa uchache, waliojinasibu kutokea “Bhughuma Ku Mwandu”.
FIRST LY CLASS OF 1973
Darasa la kwanza kumaliza la saba linatimia 1973. Sina kumbukumbu njema ya waliochaguliwa kwenda kidato cha kwanza, Lakini bila ya shaka watakua ni Robinson na Marehemu Godfrey Ndimila.
Mimi binafsi ilibidi nisubirie LY ya 1975 tulipochaguliwa pamoja na Marehemu Engineer Naftali Mjinja.
Mr Machele,
One among the first Class Seven Graduates 1973
Current Administration Building
WANAFUNZI
Kwa umri wa shule ya Msingi Namalebe, kwa wastani wa wanafunzi 45 kila mwaka, kwa kufikia mwaka wa Jubilee 2019,  Basi bila ya shaka  wanafuni zaidi ya elfu tatu watakua wamepitia hapa. Si rahisi kuwakumbuka na kuwapata wote, wengine wametangulia mbele ya haki,wapumzike kwa amani .wengine wana majukumu mazito ya kuitumikia nchi ,lakini pia wapo waliobakia vijijini mwao hawana mbele wala nyuma .Lakini kwa makala yangu hii, nawakusudia wote. Ulipitia shule ya msingi Namalebe, ulivuna nini Namalebe japo kidogo. Upo tayari kuirudishia Namalebe  kidogo kutoka kidogo ulichopata kwayo?
Tujipange kwa ajili ya Jubilee ya Namalebe ya miaka 70.
Ernest Magoti, Nyabhwire Malekela Yoel, Class of 1949, Tungura Missana Mkhoi , Class of 1963. Na kizazi cha uhuru hadi sasa.
Finias Machele, Chanika Dar Es Salaam , Benjamin Masatu, Dar Es Salaam, Nyande Misana Mkhoi, Arusha. Rusasa Matekere, Mirobo Daudi, Juma Daudi, Lusoti Chiganga, Kalega Mgeta, Shabani na Fatuma mliofanya tukajua siku za mapumziko za watu wa imani ya kiislamu , Ndaro Mnaga , Goodluck M. Ngalya a.k.a Chadema, Daudi Mkani, Sumbawanga, John Mkani , Manyonyi Alex Kasoli Zakayo Chiganga na Dada zetu niliwataja awali pamoja na wengi wengineo. Kaka Mfungo Afisa Ugani, Tarime mwanariadha mahiri, ukitoa ushauri wa matumizi ya glucose miaka hiyo.
Kama kwenye njia yako ya Elimu ulipitia Namalebe, wewe ni mdau wetu. Tutafutane.
Makala hii itawekwa mtandaoni kwa Hisani ya Blog ya Msalya MyFamily, www.msalya.blogspot.com, lakini pia itanakiliwa kwenye Ukurasa wa Facebook wa Billy K Msalya.
Wadau wetu tunaombeni m ”Share” kadri mtakavyoweza kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa wadau wengi wa Namalebe wa kizazi cha zamani na cha sasa cha dotcom.
#Toward Namalebe Platnum Jubilee 2019
# Tukumbuke tulikotoka
#Shule yangu Namalebe

No comments:

Post a Comment