Sunday, July 30, 2017

USHIKWAPO SHIKAMANA

CK Junior, all the way from Vingunguti alikuja kunijulia hali leo.
Mgonjwa kwenye hali kama hii hupaswi kuwakatisha tamaa wajulia hali wako.Nami leo ilibidi kukipa likizo fupi kitanda changu.
Naam, ilibidi kunyanyuka kupiga picha na Mgeni.
Kinyerezi kwetu, Jumapili.


SIMULIZI NYINGINE YA FAMILIA YA MAGOTI

Bw. Phillipo Malekela


Mwaka 1946, wakati Mzee Magoti Kubhoja anafikwa na umauti kwa ajali ya kushikwa na Mamba, alimwacha Mjane Bi. Nyamambala Mweya akiwa mjamzito. Lakini pia akiacha watoto sita. Kaitira, Nyamitaga, Maingu, Nyabhutwema, Mnubhi na Tereza. Muyabhi ambaye hakupata bahati ya kumuona Baba yake Mzazi uso kwa macho.
Changamoto kubwa ya kimaisha kwa familia hii ilikuwa inaanza mkondo mpya. Kaitira kijana mkubwa wa familia hakuwa ameoa, hivyo jukumu la kuwa kiongozi mkuu wa familia lilikuwa kubwa mno kwake. Bahati mbaya pia Magoti hakuwa na ndugu wa karibu upande wa Baba. Kutokana na utata wa kifo chenyewe, Mitizamo tofauti ya chuki kati ya familia ya Magoti na ile ya kina Temburu ilikuwa sasa ni dhahiri. Familia ya Magoti ilipaswa kuondoka mahala mara moja baada ya mazishi.
Mwisho wa historia ya Familia ya Magoti kijijini Namibhu.
 Kwa upande wa Mama, Magoti  akizaliwa na Nyang’oko Malandala. Nyag’oko akizaliwa pamoja na mdogo wake Nyamtondo Malandala. Nyamtondo ndiye Mama Mzazi wa Malekela Nyachemo. 
Naam, familia ya Magoti ilikuwa inaanza historia mpya ya Maisha Kijiji cha Nakatuba nyumbani kwa Malekela Nyachemo. Hapa kwa Mzee Malekela wanakutana na watoto waliokuwa wamekwisha zaliwa ambao ni Rhudia, Stephano na Nyabhwire. Baadae kwa Mama Nyamabhusi walikuja kuzaliwa Damali na Tabitha.
Tabitha Malekela, Kasahunga
 Baadae pia Mzee Malekela alilazimika kurithi familia ya Mjomba wake Mukama aliyefariki. Bi Nyalulinga alirithiwa na mpwa wa mmewe. Alikuja na watoto Matofari, Muinja na Nyanjura. Na baadae  kwa Bi Nyalulinga walizaliwa Daudi na Philipo.

Tereza alikaa muda mchache Nakatuba kabla ya yeye kwenda kulelewa Mwitende .
Mnamo mwaka 1949, Ilianzishwa shule ya Msingi ya Nakatuba. Wananchi walihamasishwa kupeleka watoto wao kujipatia elimu. Mzee Malekela aliridhia Mnubhi na Nyabhwire kuandikishwa shule. Wengine walionekana wadogo na wengine walioonekana wakubwa aliona ni akiba ya nguvu kazi. Hii ndiyo sababu mji mmoja wengine walienda shule na wengine hawakwenda.
Mnubhi baada ya kumaliza darasa la Nne Namalebe , alipata kusoma Mabhuimerafuru, Ukerewe na baadae Uganda.
Nyabhwire alifanya vizuri mitihani yake ya darasa la Nne, akachaguliwa kwenda darasa la tano na sita shule ya Bwiru jijini Mwanza.
Maingu baadae alielekea  Iramba kwa Mzee Rwanda, huko alifanikiwa kuanza shule iliyompeleka hadi Bukhima na kufanikiwa kumaliza darasa la nne.
Nyamitaga na Nyabhutwema waliolewa wakitokea nyumbani kwa Mzee Malekela. Maingu akimuoa mkewe Nyamkaruka akiwa kwa mjomba wake Mzee Rwanda.

…….mkondo mpya wa familia ya Magoti, kila mmoja na maajaliwa yake…………………………………


Shukrani Bi Penina, Ankal Mnubhi Ernest, Mwl Belly na Bi Tereza kwa kuchangia katika stori hii       

Wednesday, July 26, 2017

Friday, July 21, 2017

MAISHA HUBADILIKA

Picha ya karibuni iliyopigwa na mdau wetu Shule ya Msingi Nakatuba,
Mambo mengi yamebadilika sana,
Miongo minne iliyopita, kama ingepigwa picha kama hii,
Pengine mmoja au Hakuna ambae angeonekana amevaa viatu hapa.
Lakini leo kila mwanafunzi yumo ndani ya kiatu.
Tumetoka mbali.....................

STYLISH RIDING

A cyclist enjoying riding his One wheeler along Kawawa Road.

Wednesday, July 19, 2017

MILLY GOES TO SCHOOL

A Village girl from Nakatuba, Milly Msalya now goes to School in Dar

Monday, July 17, 2017

USIKU WA AKIDA NA PENDO

Jumamosi Usiku,
Best Choice, Tabata Aroma.
Bw. Akida Hudu na Bi Pendo Ngowi walipouaga Ukapera.

NCHI HUJENGWA NA WANANCHI

Maendeleo ya Wananchi huletwa na wananchi wenyewe,
Kikao cha kijamii cha Mtaa kwa ajili ya kujadili changamoto za mtaa.
Pamoja na Mwenyekiti, Mheshimiwa Terazzo.
Romaro Pup, Jumapili.
Kinyerezi kwetu

BURIANI MZEE WETU YOWERI MASSANO

Buriani Mzee Yoweri Massano,
Baba yetu alifikwa na Mauti tarehe 13 Julai 2017 kwa Bintiye Pendo mjini Singida alikokuwa ameenda kupatiwa matibabu.
Mwili wake ulisafirishwa tarehe 14 Julai kwenda Namhula kwa Mazishi.
Hatimae Jumamosi tarehe 15 Julai 2017 amepumzishwa kwenye makazi yake akisubiria ufufuo.
Bwana alitoa,
Bwana Ametwaa,
Jina lake Lihimidiwe.

JEMBE HALIMTUPI MKULIMA

Ni wakati wa Mavuno,
Wadau wetu wa Morogoro waliwekeza shambani,
Naam, Jembe halimtupi Mkulima.
Prof Paulsen alikuwepo shamba ku"share Experience"

Friday, July 14, 2017

KIZUNGUMKUTI

Usiombe yakukute,
Uko kwenye foleni barabarani, mbele kabisa unangojea taa za kuongozea ziruhusu.
Unagundua gari haliwezi kuwaka, hadi ufungue duka!!!
Taa zinawaka na Pi Pi Pi za washirika wa nyuma yako zinaanza.
Hakika ni kizungumkuti.
Ubungo External Alhamis jioni.

Wednesday, July 12, 2017

LALA SALAMA, KODI ZA MAJENGO

Siku zinazidi kuyoyoma,
Nyongeza ya siku ziliwekwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa ajili ya kulipia kodi za Majengo nayo inaelekea ukingoni. Bado siku mbili.
Kama kawaida foleni za kulipia zimerudi Vituo vya TRA.
Ni kizungumkuti.

BONGE LA LIFT

Bora Kufika
Tazara, Buguruni

Monday, July 10, 2017

BIRTHDAY ANNIVERSARRY

My dear granddaughter, thank you for bringing so much joy into our lives… Here’s wishing you a very happy birthday, may you have a blast!

Sunday, July 9, 2017

PEEPING MOON

Watching Rising Moon from our Sebuleni
Flamingo Garden Inn
Kinyerezi kwetu

KUTOKA MAKTABA YETU MTWARA

Back in Mid 90s
Mr & Mrs Bright and Jenniffer
Good Old Days

Saturday, July 8, 2017

DARAJA LA NYERERE

Viewing the Beauty of Mwl Nyerere Bridge.
Kigamboni, Sabasaba Day

Friday, July 7, 2017

MWENDA TEZI NA OMO.......


Naam, 
Mwenda tezi na omo hurejea ngamani.
Babu Milly amerejea tena Dar baada ya kuweko kijijini Nyakatubha kwa Mwaka na ushee.

USIKU WA MBALAMWEZI


Seye, Mwongozo.
Mbalamwezi angavu.
Sabasaba Day

Thursday, July 6, 2017

YALIYOJIRI

 Bwana Shemeji,
Maseke Mgabho amefanyiwa oparesheni yenye mafanikio ya kumondolea tatizo la Kidole Tumbo lililokuwa likimsumbua, Hospitali ya Rufaa Dodoma leo.
Tumwombee uponyaji wa Haraka.
Bwana Makubhi, Mzee wa Makamuzi akiwa safarini kutoka Bunda leo gari alilokuwa akisafiria lilikubwa na dhahama ya kukamatwa kwa kosa la kusafirisha mihadharati.
Bwana Makubhi, kama abiria wengine alijitokeza kupaza sauti kuhoji sababu ya kucheleweshwa.
Lahaula,
Amejikuta akiunganishwa kwenye kesi ya kusafirisha mihadharati na kuswekwa mahabusu.
Upelelezi baadae imeonekana hana hatia.
Gari na abiria limeruhusiwa kuendelea na safari baada ya kuletwa Dereva na Kondakta wengine.

BIRTHDAY ANNIVERSARY

Dear Ted,
I tried the google to find the perfect wish for you on your special day. But trust me, nothing grabbed my attention. So, I decided to send this greeting to you – “Be happy always”.

Wednesday, July 5, 2017

NAKATUBA FROM OUR LIBRARY

Vijana wa Zamani,
Ni Mwaka 1957, Picha ya Kumbukumbu Harusi ya Majige Somba (Katikati, Msitari wa mbele) na Bi Nyakejirabhi (Kushoto kwa Bw. Harusi). 
Wengine pichani waliosimama kutoka kushoto.
Late Matofali Mkama
Late Mafuru Makene
Mr Ndaro Magolinya aka Bayi Murji
Late CK Msalya aka Sike Patel

Picha kwa hisani ya Mdau wa Blog. Mr. Nyachiriga

Tuesday, July 4, 2017

Monday, July 3, 2017

WEEK ENDING IN STYLE

Kupanga ni Kuchagua,
Samunge Kwetu
Jumapili.

SUZZY SEND OFF COUNT DOWN

Kikao cha Nne,
Maandalizi Send Off ya Suzzy Nyanguli.
Flamingo Garden Inn, Jumapili.