Sunday, July 30, 2017

SIMULIZI NYINGINE YA FAMILIA YA MAGOTI

Bw. Phillipo Malekela


Mwaka 1946, wakati Mzee Magoti Kubhoja anafikwa na umauti kwa ajali ya kushikwa na Mamba, alimwacha Mjane Bi. Nyamambala Mweya akiwa mjamzito. Lakini pia akiacha watoto sita. Kaitira, Nyamitaga, Maingu, Nyabhutwema, Mnubhi na Tereza. Muyabhi ambaye hakupata bahati ya kumuona Baba yake Mzazi uso kwa macho.
Changamoto kubwa ya kimaisha kwa familia hii ilikuwa inaanza mkondo mpya. Kaitira kijana mkubwa wa familia hakuwa ameoa, hivyo jukumu la kuwa kiongozi mkuu wa familia lilikuwa kubwa mno kwake. Bahati mbaya pia Magoti hakuwa na ndugu wa karibu upande wa Baba. Kutokana na utata wa kifo chenyewe, Mitizamo tofauti ya chuki kati ya familia ya Magoti na ile ya kina Temburu ilikuwa sasa ni dhahiri. Familia ya Magoti ilipaswa kuondoka mahala mara moja baada ya mazishi.
Mwisho wa historia ya Familia ya Magoti kijijini Namibhu.
 Kwa upande wa Mama, Magoti  akizaliwa na Nyang’oko Malandala. Nyag’oko akizaliwa pamoja na mdogo wake Nyamtondo Malandala. Nyamtondo ndiye Mama Mzazi wa Malekela Nyachemo. 
Naam, familia ya Magoti ilikuwa inaanza historia mpya ya Maisha Kijiji cha Nakatuba nyumbani kwa Malekela Nyachemo. Hapa kwa Mzee Malekela wanakutana na watoto waliokuwa wamekwisha zaliwa ambao ni Rhudia, Stephano na Nyabhwire. Baadae kwa Mama Nyamabhusi walikuja kuzaliwa Damali na Tabitha.
Tabitha Malekela, Kasahunga
 Baadae pia Mzee Malekela alilazimika kurithi familia ya Mjomba wake Mukama aliyefariki. Bi Nyalulinga alirithiwa na mpwa wa mmewe. Alikuja na watoto Matofari, Muinja na Nyanjura. Na baadae  kwa Bi Nyalulinga walizaliwa Daudi na Philipo.

Tereza alikaa muda mchache Nakatuba kabla ya yeye kwenda kulelewa Mwitende .
Mnamo mwaka 1949, Ilianzishwa shule ya Msingi ya Nakatuba. Wananchi walihamasishwa kupeleka watoto wao kujipatia elimu. Mzee Malekela aliridhia Mnubhi na Nyabhwire kuandikishwa shule. Wengine walionekana wadogo na wengine walioonekana wakubwa aliona ni akiba ya nguvu kazi. Hii ndiyo sababu mji mmoja wengine walienda shule na wengine hawakwenda.
Mnubhi baada ya kumaliza darasa la Nne Namalebe , alipata kusoma Mabhuimerafuru, Ukerewe na baadae Uganda.
Nyabhwire alifanya vizuri mitihani yake ya darasa la Nne, akachaguliwa kwenda darasa la tano na sita shule ya Bwiru jijini Mwanza.
Maingu baadae alielekea  Iramba kwa Mzee Rwanda, huko alifanikiwa kuanza shule iliyompeleka hadi Bukhima na kufanikiwa kumaliza darasa la nne.
Nyamitaga na Nyabhutwema waliolewa wakitokea nyumbani kwa Mzee Malekela. Maingu akimuoa mkewe Nyamkaruka akiwa kwa mjomba wake Mzee Rwanda.

…….mkondo mpya wa familia ya Magoti, kila mmoja na maajaliwa yake…………………………………


Shukrani Bi Penina, Ankal Mnubhi Ernest, Mwl Belly na Bi Tereza kwa kuchangia katika stori hii       

1 comment:

  1. These are wonderful stories that should be compiled and keep in durable record facilities to be read by many generations in future.

    ReplyDelete