Thursday, July 6, 2017

YALIYOJIRI

 Bwana Shemeji,
Maseke Mgabho amefanyiwa oparesheni yenye mafanikio ya kumondolea tatizo la Kidole Tumbo lililokuwa likimsumbua, Hospitali ya Rufaa Dodoma leo.
Tumwombee uponyaji wa Haraka.
Bwana Makubhi, Mzee wa Makamuzi akiwa safarini kutoka Bunda leo gari alilokuwa akisafiria lilikubwa na dhahama ya kukamatwa kwa kosa la kusafirisha mihadharati.
Bwana Makubhi, kama abiria wengine alijitokeza kupaza sauti kuhoji sababu ya kucheleweshwa.
Lahaula,
Amejikuta akiunganishwa kwenye kesi ya kusafirisha mihadharati na kuswekwa mahabusu.
Upelelezi baadae imeonekana hana hatia.
Gari na abiria limeruhusiwa kuendelea na safari baada ya kuletwa Dereva na Kondakta wengine.

No comments:

Post a Comment