Friday, May 12, 2017

TEMBEA UJIONEE


 Kisiwa kidogo cha Okinoshima, mji wa Munakata, Fukuoka Japan.
Kisiwa kina eneo la Ekari 240, na kiko katika mwinuko unaofikia Mita 244
 Kisiwa hiki kinachukuliwa kama pahala patakatifu, Mwanamke yeyote ni marufuku kukanyaga kisiwani hapa. Hairuhusiwi kuchukua kitu chochote toka kisiwani hata iwe jani la mmea.Na hata wanaume wanaotembelea hapa hutakiwa kwanza kubakia utupu na kufanya ibada ya Utakaso, na kamwe hawaruhusiwi kufichua maelezo ya safari yao.
 Kisiwa kwa sasa kinakaliwana mtu mmoja tu. Na huyu ni mhudumu wa hapa, Mtumishi wa Mamlaka ya mji wa Munakata Taishi.
Kisiwa cha Okinoshima.

Source:Wikipedia and Alistair Coleman (BBC)

No comments:

Post a Comment