Tuesday, October 25, 2016

TETE A TETE

Kuteta na Ankal,
Kinyerezi kwetu, Sunday.

Monday, October 24, 2016

SIMULIZI YA MAGOTI KUBHOJA

 Kaitila Magoti Kubhoja, The first born- Mabhuimerafuru
Mrs Nezia Maingu Magoti - Karukekere
Tereza Magoti (Mrs Wilson Kuruchumila) - Kibara
 Nyamaira kubhoja na Magoti Jnr (Blogger) - Igundu
 Nyamitaga Neema Magoti (Mrs Chisute Mteki) - Bhulinga
 Ernest Munubhi Magoti - Mabhuimerafuru




Nimekuwa nikitatizwa,
Simulizi zimekuwa zikieleza Magoti Kubhoja alikuwa na maskani yake Kibara, Namibu hadi alipokutwa na mauti.
Kaitila Magoti, mwanae wa kwanza maskani yake yako Mabhui Merafuru hadi leo, na Maingu Magoti maskani yake hadi anapatwa na mauti yalikuwa Karukekere, Chingurubhira.

Karibuni nilipata likizo ambayo ilinifikisha hadi Igundu, Majita Mabhui Merafuru na Karukekere, na nilipata nafasi  ya kudodosa kutoka kwa watu wa familia yake kulikoni wanae kuacha pahala pa asili!

Tafadhali fuatana nami katika simulizi hii ya Bw Magoti Kubhoja.

Hakuna tarehe kamili ya kuzaliwa kwa Magoti, lakini inakisiwa kuwa huenda alizaliwa kwenye miaka ya mwanzo ya karne ya 19. Alizaliwa katika kijiji cha Ekome na kukulia hapo miaka ya awali. Hakuna hakika ya asili yao, japo kulikuwa na fununu kuwa chimbuko lao hasa walitokea Buhaya. Lakini amekua akijulikana kama Mjita Mkome, ukoo wa  Abhakura – Wa kutoka mbali.

Wakati wa ujana wake, Magoti alipendelea kwenda kukaa Iramba, Sikiro kwa mjomba wake Bw. Mukama Marandara, kaka yake na Nyang’oko. Inasimuliwa kwamba siku moja Shangazi zake akiwepo mmoja aliyeitwa Nyamtondo walikwenda kumtembelea Kubhoja  huko Ekome. Hawakupendezwa kumuona Kaka yao akijiandalia kukoka moto wa jioni “Echoto” kwa kuwa Magoti hakuwepo. Waliahidi kumshughulikia. Huko Sikiro Magoti alikosa nguvu za kiume na akalazimika kurejea Ekome kwa matibabu.
Miaka mingi baadae baada ya kifo cha Kubhoja alirejea  Iramba,Sikiro, lakini safari hii hakukaa sana kwa sababu alishawishiwa na Binamu yake Bw. Temburu mtoto wa shangazi yake Nyakalolo kwenda kuishi Namibu jambo aliloliridhia wakaongozana kwenda huko ambako Temburu alimpatia mashamba. Akiwa Namibu Bw Magoti alimwoa Nyamkubhi Bhulilo mkazi wa Majita Bhutata. Ni wakati huu kulipoanza kujitokeza tofauti kati yake na Binamu yake hivyo akawa amedhamiria kuanza mji wake.

Kwa upande wake Bw Temburu pamoja na kuoa mapema hakuwa amejaaliwa kupata watoto. Na katika kuhangaikia kupata watoto alifika hadi kwa waganga wa Kikara waliokubali kumsaidia ila kwa kumtoa kafara nduguye wa karibu, Temburu aliridhia kafara yake kuwa Bw. Magoti.

Magoti baada ya kuanza kuwepo  kwa tofauti na binamu yake Bw. Temburu alikuwa amedhamiria kuanzisha mji wake. Siku moja katika maandalizi ya ujenzi wa mji wake alikuwa amepanga na shemeji yake mme wa Nyamaira “Nyakubhoja” kuwa  angemletea baadhi ya vifaa vya kusaidia ujenzi kesho yake. Aliamua yeye na mwanae Maingu kwenda ziwani jioni hiyo kuwatafutia mboga ya kesho yake, Hakurejea tena.
Wakiwa uvuvini, Magoti aliopolewa na Mamba kutoka mtumbwini akimwacha Maingu pekee. Habari zilisambaa na jitihada zikafanyika usiku kucha kumtafuta huyo Mamba mla watu. Hakupatikana.
Lakini kesho yake maiti ya Magoti ilipatikana ufukweni mwa ziwa ikiwa na majeraha ya damu. Ikiwa imerudishwa na Mamba mla watu, na ndio ulikuwa mwisho wa Magoti Kubhoja. Mnamo mwaka wa 1946.
Miaka ya baadae Temburu alifanikiwa kupata watoto, Mmoja wao maarufu kama Mwinyi Temburu anaendelea  kuishi maeneo yaleyale yaliyoachwa na Temburu na Magoti pale Kibara Namibu hadi leo.



………………………………………………………fuatana nami wakati mwingine……….

Friday, October 21, 2016

HOME IS THE BEST

Majumba Sita, Ukonga
Kinyerezi Bus Stand

MBUZI WA MASKINI HAZAI

Msimbazi Centre, Kawawa Road
Recently

DEREVA MAKINI

FANYA HAYA UNAPOKUWA BARABARANI:
1. Washa indiketa unapotaka kutoka barabarani au kuruhusu gari lipite angalau 50m kabla ya kutoka.
2. Ukiona mwenzako ana ovateki, usimfuate/ kuunganisha hadi ujiridhishe kuwa ni salama.
3. Kuwasha indiketa sio kibali cha kukuruhusu upite/ kupinda kulia, ila ni ishara kuwa unataka kupinda, hivyo ukishawasha, sharti uangalie nyuma (side mirror) na mbele, kujiridhisha kuwa ni salama kabla ya kupinda.
4. Usikimbize gari mahali ambako huoni umbali mrefu/ kwenye Bonde au Kona, kwani huwezi jua nini unaweza kukutana nacho huko (wanyama, gari imeharibika nk)
5. Mkiwa mnafuatana (magari mawili) mwenzako akasimama, usimpite kabla ya kujua kwa nini amesimama.
6. Kuendesha chini ya 50Km kwa saa highway, haikuepushii ajali bali ni kuwapa usumbufu watumia barabara wenzako; cha msingi ni kufuata taratibu za barabarani.
7. KUMBUKA kukimbiza gari sio chanzo cha msingi cha kuleta ajali; Kinacholeta ajali ni kutokujua sheria au kutozifuata sheria na alama za barabarani zinazokuruhusu wapi ukimbize na wapi uende polepole.
8. Usiongee na simu lakini pia usipige sana stori au Kusikiliza radio/mahubiri kwenye radio wakati hujazoea kwani ukinogewa unaweza kujisahau na kukwangua/kukwanguliwa
9. Jitahidi kujua ukubwa wa gari lako, hasa kama unarudi nyuma au unapita sehemu nyembamba; omba msaada wa kuelekezwa.
10. Ukipaki gari barabarani, hakikisha ni salama kabla ya kufungua Mlango. Hii ni jukumu lako kuangalia usalama wako na uliowapakia hasa kama mlango unafungukia kulia (upande wa barabarani).
11. KUMBUKA kuna bodaboda zinazoweza kugonga mtu anayeshuka kwa urahisi.

Wednesday, October 12, 2016

Tuesday, October 11, 2016

KIFO

Tuna na paswa kufanya nini wakati mauti yako machoni mwetu? Ikiwa Mungu yu pamoja nasi tusiwe na hofu imeandikwa Zaburi 23:4 "Naam nijapopita kati ya ponde lauvuli wa mauti sitaogopa mabaya kwa maana wewe upo pamoja nami gongo lako na fimbo yako vyanifariji."
Kifo kinafanana vipi? Nikama usingizi. imeandikwa 1Wathesalonike 4:13 "Lakini ndugu hatutaki msijue habari za waliolala mauti msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini." pia Yohana 11:11-14 "Iliyasema hayo kisha baada ya hayo akawaambia, rafiki yetu Lazaro, amelala lakini nitakwenda nipate kumwamsha. Basi wale wanafunzi wakamwambia Bwana ikiwa amelala tapona lakini Yesu alikuwa amenena habari ya mauti yake nao walidhani yakuwa ananena habari ya kulala usingizi. Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi Lazaro amekufa."
Danieli amesema nini kuhusu kifo? Imeandikwa Danieli 12:2 "Tena wengi wahao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka wengine wapate uzima wa milele wengine aibu na kudharauliwa milele."
Je? walio kufa wanajua lolote? Imeandikwa Mhubiri 9:5-6, 10Kwa sababu walio hai wanjua ya kuwa watakufa lakini wafu hawajui neno lolote wala hawana ijara tena maana kumbukumbu lao limesahauliwa mapenzi yao namachukio yao na husuda yao imepotea yote pamoja wala hawana sehemu tena katika jambo lolote lililofanyika chini ya jua, lolote mkono wako utakapolipata kulifanya ulifanye kwa nguvu zako kwa kuwa hakuna kazi wala shauri wala maarifa wala hekima huko kuzimu uwendako wewe."
Kifo sio mwisho! Imeandikwa Isaya 26:19 "Wafu wako wataishi maiti zako zitafufuka amkeni kaimbe ninyi mnao kaa mavumbini kwa maana umande wako nikama umande wa mimea nayo ardhi itawatoa waliokufa."
Yesu ametuhaidi nini kuhusu kifo? imeandikwa Hosea 13:14 "Nitawakomboa na nguvu za kaburi nitawaokoa na mauti ewe mauti yawapi mapigo yako? Ewe kaburi ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafishwa na macho yangu."
Ufufuwaji uko katika nguvu za Mungu imeandikwa 1Wakorintho 15:21-22 "Maana ya kuwa mauti ili letwa na mtu kadhalika na kiyama ya wafu italetwa na mtu kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa kadhalika na katika Kristo wate wanahuishwa."
Mungu alimpa mwanawe kwa sababu gani? imeandikwa Yohana 3:16 " Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenada ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee ila kila amwaminiye asipotee bali awena uzima wamilele."
Watu wema na wabaya watafufuliwa siku ya kiama imeandikwa Yohana 5:28-29 "Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote walio makaburini wataisikia sauti yake nao watatoka wao waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima na wale walio tenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu".
Waaminifu watafufuliwa yesu akirudi mara ya pili imeandikwa 1Wathesalonike 4:16-18 "Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbiguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu na parapanda ya mungu nao walio kufa katika kristo watafufuliwa kwanza kisha sisi tulio hai tuliosalia tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu ili tumlaki Bwana hewani na hivyo tutakuwa na Bwana milele. Basi farijianeni kwa maneno hayo."
Tutafanana vipi baada ya ufufuo? Imeandikwa Wafilipi 3:20-21 "Kwa maana sisi wenyeji wetu uko mbinguni kutoka huko tunamtazamia mwokozi Bwana wetu yesu kristo atakaye ubadili mwili wetu wa unyonge upate kufanana na mwili wake wa utukufu kwa uweza ule ambao kwa huo uweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake."
Watakatifu wataishi mda gani? imeandikwa Luka 20:36 "Wala hawawezi kufa tena, kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo."
Wenye dhambi wta ngoja kwa mda gani kabla ya kiama? imeandikwa Ufunuo 20:4-5, 9 "Kisha nikaona vitu vya enzi wakaketi juu yake nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya uchuhuda wa Yesu... Hao walio wafu salia hawakuwa hai hataitimie ile miaka elfu,... 9 Moto ukachika toka juu mbiguni ukawateketeza."
Wenye dhambi ni nani? imeandikwa Ufunuo 21:8 "Bali waoga, wasioamini, wachukizao, wauwaji, wazinzi, wachawi, waabuduo sanamu, na waongo sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti, hiyo ndiyo mauti ya pili."


AHSANTE KIBOKO

Shading for the needy,
Mikocheni, Mwai Kibaki Road

NAMPANGALA GRAVE YARD

Wamemaliza kazi, na sasa wamepumzika.
Wapendwa wetu,
Shangazi Mtundu,
Kaka Kururetera
Kaka Iddi
Kaka Hatari
Wamepumzika hapa.......................

Brief stop over on my way from Nansio to Nyakatubha.

Thursday, October 6, 2016

PHOTOS FROM BHULINGA

Trip to Majita Bhulinga
September

Wednesday, October 5, 2016

NAKATUBA TRIP

Nyachiriga and Family at JKNIA, Dar Es Salaam.
Before boarding Fast Jet en-route to Mwanza, Bunda and Nakatuba. 

Tuesday, October 4, 2016

HAPA STORI TU

Kijiwe cha Mjunguti,
Stori zote za Nyakatuba utazipata hapa.
Ni kijiwe cha stori tu, hakuna msosi.
Kwa ajili ya msosi kila mtu huondoka kwa muda wake.

SUNSET IN IGUNDU

Madhari nzuri jua likizama katika kijiji cha Igundu.
Tumefika kumtembelea Nyamaila, mdogo wake na Magoti.

Monday, October 3, 2016

LIGI YA KUKU

Ni ligi ya kugombea kuku kwa vijana chini ya 15,
Chandimu ndiyo mpira wetu hapa, lakini ukiangalia kuna Vipaji dhahiri vinaonekana.
Kisichojulikana ni lini wataonwa.
Mimi nilishabikia Kurugongo, Barcelona wa Nakatuba,
Watoto wa Centre waliondolewa na Namalebe waliokuja baadae kuchukua Kombe "Kuku"

NI CHEREKO

Ni chereko chereko,
Bwana amepata Bibi,
na Bibi amepata Bwana,
Ni Furaha na vigelegele,
Ni kula kunywa na kucheza.
Ni kwetu Nakatuba.