Friday, October 21, 2016

DEREVA MAKINI

FANYA HAYA UNAPOKUWA BARABARANI:
1. Washa indiketa unapotaka kutoka barabarani au kuruhusu gari lipite angalau 50m kabla ya kutoka.
2. Ukiona mwenzako ana ovateki, usimfuate/ kuunganisha hadi ujiridhishe kuwa ni salama.
3. Kuwasha indiketa sio kibali cha kukuruhusu upite/ kupinda kulia, ila ni ishara kuwa unataka kupinda, hivyo ukishawasha, sharti uangalie nyuma (side mirror) na mbele, kujiridhisha kuwa ni salama kabla ya kupinda.
4. Usikimbize gari mahali ambako huoni umbali mrefu/ kwenye Bonde au Kona, kwani huwezi jua nini unaweza kukutana nacho huko (wanyama, gari imeharibika nk)
5. Mkiwa mnafuatana (magari mawili) mwenzako akasimama, usimpite kabla ya kujua kwa nini amesimama.
6. Kuendesha chini ya 50Km kwa saa highway, haikuepushii ajali bali ni kuwapa usumbufu watumia barabara wenzako; cha msingi ni kufuata taratibu za barabarani.
7. KUMBUKA kukimbiza gari sio chanzo cha msingi cha kuleta ajali; Kinacholeta ajali ni kutokujua sheria au kutozifuata sheria na alama za barabarani zinazokuruhusu wapi ukimbize na wapi uende polepole.
8. Usiongee na simu lakini pia usipige sana stori au Kusikiliza radio/mahubiri kwenye radio wakati hujazoea kwani ukinogewa unaweza kujisahau na kukwangua/kukwanguliwa
9. Jitahidi kujua ukubwa wa gari lako, hasa kama unarudi nyuma au unapita sehemu nyembamba; omba msaada wa kuelekezwa.
10. Ukipaki gari barabarani, hakikisha ni salama kabla ya kufungua Mlango. Hii ni jukumu lako kuangalia usalama wako na uliowapakia hasa kama mlango unafungukia kulia (upande wa barabarani).
11. KUMBUKA kuna bodaboda zinazoweza kugonga mtu anayeshuka kwa urahisi.

No comments:

Post a Comment