Monday, October 24, 2016

SIMULIZI YA MAGOTI KUBHOJA

 Kaitila Magoti Kubhoja, The first born- Mabhuimerafuru
Mrs Nezia Maingu Magoti - Karukekere
Tereza Magoti (Mrs Wilson Kuruchumila) - Kibara
 Nyamaira kubhoja na Magoti Jnr (Blogger) - Igundu
 Nyamitaga Neema Magoti (Mrs Chisute Mteki) - Bhulinga
 Ernest Munubhi Magoti - Mabhuimerafuru




Nimekuwa nikitatizwa,
Simulizi zimekuwa zikieleza Magoti Kubhoja alikuwa na maskani yake Kibara, Namibu hadi alipokutwa na mauti.
Kaitila Magoti, mwanae wa kwanza maskani yake yako Mabhui Merafuru hadi leo, na Maingu Magoti maskani yake hadi anapatwa na mauti yalikuwa Karukekere, Chingurubhira.

Karibuni nilipata likizo ambayo ilinifikisha hadi Igundu, Majita Mabhui Merafuru na Karukekere, na nilipata nafasi  ya kudodosa kutoka kwa watu wa familia yake kulikoni wanae kuacha pahala pa asili!

Tafadhali fuatana nami katika simulizi hii ya Bw Magoti Kubhoja.

Hakuna tarehe kamili ya kuzaliwa kwa Magoti, lakini inakisiwa kuwa huenda alizaliwa kwenye miaka ya mwanzo ya karne ya 19. Alizaliwa katika kijiji cha Ekome na kukulia hapo miaka ya awali. Hakuna hakika ya asili yao, japo kulikuwa na fununu kuwa chimbuko lao hasa walitokea Buhaya. Lakini amekua akijulikana kama Mjita Mkome, ukoo wa  Abhakura – Wa kutoka mbali.

Wakati wa ujana wake, Magoti alipendelea kwenda kukaa Iramba, Sikiro kwa mjomba wake Bw. Mukama Marandara, kaka yake na Nyang’oko. Inasimuliwa kwamba siku moja Shangazi zake akiwepo mmoja aliyeitwa Nyamtondo walikwenda kumtembelea Kubhoja  huko Ekome. Hawakupendezwa kumuona Kaka yao akijiandalia kukoka moto wa jioni “Echoto” kwa kuwa Magoti hakuwepo. Waliahidi kumshughulikia. Huko Sikiro Magoti alikosa nguvu za kiume na akalazimika kurejea Ekome kwa matibabu.
Miaka mingi baadae baada ya kifo cha Kubhoja alirejea  Iramba,Sikiro, lakini safari hii hakukaa sana kwa sababu alishawishiwa na Binamu yake Bw. Temburu mtoto wa shangazi yake Nyakalolo kwenda kuishi Namibu jambo aliloliridhia wakaongozana kwenda huko ambako Temburu alimpatia mashamba. Akiwa Namibu Bw Magoti alimwoa Nyamkubhi Bhulilo mkazi wa Majita Bhutata. Ni wakati huu kulipoanza kujitokeza tofauti kati yake na Binamu yake hivyo akawa amedhamiria kuanza mji wake.

Kwa upande wake Bw Temburu pamoja na kuoa mapema hakuwa amejaaliwa kupata watoto. Na katika kuhangaikia kupata watoto alifika hadi kwa waganga wa Kikara waliokubali kumsaidia ila kwa kumtoa kafara nduguye wa karibu, Temburu aliridhia kafara yake kuwa Bw. Magoti.

Magoti baada ya kuanza kuwepo  kwa tofauti na binamu yake Bw. Temburu alikuwa amedhamiria kuanzisha mji wake. Siku moja katika maandalizi ya ujenzi wa mji wake alikuwa amepanga na shemeji yake mme wa Nyamaira “Nyakubhoja” kuwa  angemletea baadhi ya vifaa vya kusaidia ujenzi kesho yake. Aliamua yeye na mwanae Maingu kwenda ziwani jioni hiyo kuwatafutia mboga ya kesho yake, Hakurejea tena.
Wakiwa uvuvini, Magoti aliopolewa na Mamba kutoka mtumbwini akimwacha Maingu pekee. Habari zilisambaa na jitihada zikafanyika usiku kucha kumtafuta huyo Mamba mla watu. Hakupatikana.
Lakini kesho yake maiti ya Magoti ilipatikana ufukweni mwa ziwa ikiwa na majeraha ya damu. Ikiwa imerudishwa na Mamba mla watu, na ndio ulikuwa mwisho wa Magoti Kubhoja. Mnamo mwaka wa 1946.
Miaka ya baadae Temburu alifanikiwa kupata watoto, Mmoja wao maarufu kama Mwinyi Temburu anaendelea  kuishi maeneo yaleyale yaliyoachwa na Temburu na Magoti pale Kibara Namibu hadi leo.



………………………………………………………fuatana nami wakati mwingine……….

No comments:

Post a Comment