Wednesday, May 16, 2012

WEEKEND KIZUNGUMKUTI

Jumamosi iliyoanza vizuri siku hii ilimalizika vibaya baada ya kukumbwa na tafrani ya kugongwa na Bodaboda, mitaa ya njiapanda ya segerea/Majumbasita
Ikanilazimu kupata uchunguzi Mico Airport Hospital
Pamoja na Mhanga mwenzangu.
Kwani baada ya kugongwa mimi, Rubani alisepa. Lakini hatua kadhaa baadae kabla ya kuingia barabara kuu akamgonga mwingine na hapo ikawa mwisho wa safari. Japo alifanikiwa kusepa tena, Bodaboda yake ilibakia.
Nikapata dawa za maumivu
Nikitafakari jinsi nilivyonusurika, hakika Mungu ni Mwema na anipenda
Hapa ndio pahala penyewe iliponikuta tafrani
Jumapili asubuhi, mhanga mwingine tena wa bodaboda
Pahala, ni nyumbani kabisa hapa kwetu Kinyerezi
Wadau waliokuwa wamekuja kumuona mgonjwa No 1, ikawalazimu kumpeleka mhanga huyu
na kumhudumia
Lakini mdau huyu, pengine sababu ya mazoezi mengi, mara baada ya kurejea alijichanganya haraka na kuwa busy bila habari ya yaliyomsibu

No comments:

Post a Comment